Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe,amekemea
vikali tabia ya baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba,kuzomeana. Mbowe
alisema kwa hali ilipofikia, kuna haja kwa kila chama kuwapa semina
wajumbe wake, ili walione Bunge hilo kuwa ni la kitaifa na siyo kikao
cha chama cha siasa.
“Kuzomeana
ni mambo ya kitoto, siwezi kupongeza utovu wa hali ya juu wa nidhamu
ulioonyeshwa na baadhi ya wajumbe. Tukiruhusu zomeazomea, itakuwa sawa
na genge la wahuni,” alisema Mbowe. Mbowe
ambaye pia ni mjumbe wa Bunge hilo alisema,
kuna mambo ya msingi
yanapingwa tu kwa sababu yametolewa na mjumbe kutoka chama fulani cha
siasa bila kuangalia mantiki ya hoja. “Ni
kweli kiti kinayumba nafasi ya kuchangia inatolewa kwa upendeleo,lakini
hiyo haiwezi kuwa sababu ya sisi kushindwa kuheshimiana na kuheshimu
mawazo ya wengine,”alisema Mbowe na kuongeza;
“Kuna umuhimu wa vyama vyetu kurudi na kukaa na wajumbe wetu kwa
sababu mvutano mkubwa hauko kwenye lile kundi la watu 201 ni vyama vya
siasa,”alisema. Kwa
mujibu wa Mbowe,kama Bunge hilo halitatunga kanuni kali ili kila mjumbe
aheshimu mawazo ya wenzake na kuruhusu kila mjumbe, aseme bila
utaratibu ni vurugu. Mbowe
alisema kinachotokea ndani ya Bunge hilo kwa baadhi ya wajumbe kufanya
mambo aliyoyaita ni ya kitoto ikiwamo kuzomea, ni kujidhalilisha na
kushusha hadhi ya chombo hicho muhimu
0 comments:
Post a Comment