Bwana Kabbah anasifiwa zaidi duniani kwa kurejesha amani nchini Sierra Leone baada ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Amefariki nyumbani kwake akiwa na miaka
82.Alhaji Ahmad Tejan Kabbah alizaliwa February 16, 1932. Aliongoza
Sierra Leone kati ya mwaka wa 1996 hadi 1997 na kisha tena mwaka wa 98
hadi mwaka wa 2007.
Katika
miaka mingi ya utu uzima wake, alihudumu kama mtaalamu wa uchumi na
sheria. Alifanya kazi kwa miaka mingi na shirika la maendeleo la Umoja
wa mataifa UNDP. Baada ya kujiuzulu kutoka umoja huo mwaka wa 92,
alirudi zake nchini Sierra Leone na kujiingiza katika siasa za nchi
hiyo.
Maisha yake ya siasa
Mnamo mwaka wa tisini na sita, bwana Kabbah
alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama Sierra Leone's People's Party (SLPP)
na kuwania urais kwa tikiti ya chama hicho mwaka wa 96.
Katika kinyanganyiro hicho, alishinda na kuwa
rais kwa 59% ya kura na kumpiku mpinzani wake mkuu John Karefa-Smart wa
chama cha United National People's Party (UNPP) aliyepata 40% tu ya
kura.
Waangalizi wa kimataifa walitangaza kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.
Kikubwa atakachokumbukwa nacho ni hotuba yake ya
kuapishwa mjini Freetown, alipoahidi kumaliza kabisa mapigano ya
wenyewe kwa wenyewe, jambo alilotekeleza baada ya kuwa rais.
Bwana Kabbah ni wa kabila la Mandingo kiasilia
na ndiye aliyekuwa rais wa kwanza wa kiislamu wa Sierra Leone. Alizaliwa
katika kijijji cha Pendembu, wilaya ya Kailahun mashariki mwa Sierra
Leone, japo udogoni mwake alikulia mji mkuu wa Free town.
Utawala wa Kabbah
Sehemu kubwa ya uongozi wa Kabbah ilishawishiwa
na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyotokea nchini Sierra Leone kwa
muda mrefu, huku akikumbwa na mapinduzi ya muda yaliyofanywa na
wanamgambo wa United Front wakiongozwa na Foday Sankoh. Mapinduzi hayo
yalim'ngoa madarakani kati ya Mei 97 hadi March 98.
Hata hivyo alirejeshwa madarakani kufuatia
usaidizi wa kijeshi kutoka kikosi cha Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika
Magharibi (ECOWAS) kilichoongozwa na Nigeria.
Awamu ya pili ya machafuko ya ndani na mauaji
ilisababisha kuingiliwa na Umoja wa mataifa pamoja na Uingereza nchini
humo mwaka wa 2000.
Harakati za amani
Katika wadhifa wake kama rais, Kabbah alianzisha
mazungumzo na wanamgambo hao wa RUF ili kumaliza mapigano hayo ya
ndani. Alisaini mikataba kadhaa ya kusitisha mapigano na kiongozi wa
waasi Foday Sankoh, ukiwemo ule mkataba wa mwaka wa 1999 wa mjini Lome'
ambapo kwa mara ya kwanza waasi hao walitekeleza na kusitisha kabisa
mapigano na mashambulio dhidi ya serikali.
Na pale mkataba huo ulipovunjika baadaye, Kabbah
alifanya kampeini kuomba usaidizi kutoka Umoja wa Mataifa, Uingereza,
Jumuiya ya ECOWAS na hata Muungano wa Afrika, AU ili kurejesha amani.
Kabbah alitagaza rasmi kumalizika kwa vita vya
ndani vya Sierra Leone mwaka wa 2002. Maelfu ya raia wa Sierra Leone
walikimbia katika barabara kuu za nchi hiyo kusherehekea hatimaye
kupatikana amani.
Miaka michache baadaye Kabbaha alipata ushindi
wa rahisi sana kuongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano
alipopata 70% ya kura na kumpiku mpinzani wake mkuu Ernest Bai Koroma wa
chama cha All People's Congress (APC).
Hapo pia, waangalizi wa kimataifa walitangaza uchaguzi kuwa huru na wa haki.
Hapo pia, waangalizi wa kimataifa walitangaza uchaguzi kuwa huru na wa haki.
0 comments:
Post a Comment