WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe,
amekikejeli Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba kinaufanya uchaguzi wa rais
kama uchaguzi wa kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani (Papa).
Membe alitolea mfano wa uchaguzi wa Papa jana wakati akijibu maswali
ya waandishi wa habari waliotaka kupata maoni na hatima yake kisiasa,
baada ya CCM kumfungia kwa miezi 12 na kumuweka chini ya uangalizi,
baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kukiuka kanuni za chama hicho kwa
kuanza mbio za urais mwaka 2015 mapema.
Waziri Membe alisema kuwa mataifa mengi duniani yameiga mambo mengi
yakiwemo mavazi ya majaji, wanasheria na spika wa bunge kutoka utamaduni
wa Kirumi unaotumiwa na kanisa hilo, lakini yameshindwa kuiga uchaguzi
wa Papa.
0 comments:
Post a Comment