Inawezekana wakati unatembea njiani ukaona wanaume au watoto wadogo wa kiume wakiwa na matiti tena makubwa ambapo watu wengi huchukulia kama ni kawaida. Kitaalamu, tatizo hilo hujulikana kama, gynecomastia nalo ni kukua kuliko kawaida kwa tishu ya kwenye titi inayojulikana kama glandular tissue.
Tatizo hili huonekana zaidi kwa watoto wachanga
na wanaume walio katika umri wa kubalehe, lakini pia huonekana kwa watu
wazima na wazee.
Ukubwa wa tatizo
Asilimia 60-90 ya watoto wachanga wanapata tatizo
hili la kukua kwa matiti kwa mpito linalojulikana kitaalamu kama,
transient gynecomastia kutokana na kuwepo kwa kichocheo cha aina ya
estrogen kwa wingi wakati wa ujauzito wa mama.
Kati ya asilimia 4-69 ya vijana walio katika umri
wa kubalehe imeonekana wanapata tatizo hili kutokana na kuwepo kwa
wingi kwa kimeng’enyo aina ya estradiol. Mara nyingi huonekana katika
umri kati ya miaka 10-12 na hupotea taratibu ndani ya miezi 18, si
kawaida yake kuonekana kwa vijana walio na umri wa zaidi ya miaka 17.
Asilimia 24-65 ya watu wazima hupatwa na tatizo
hili, hii hutokana na kubadilishwa kwa wingi kwa kichocheo aina ya
testosterone kuwa estradiol na kutolewa kwa uchache kwa kichocheo hiki
cha testosteron kutoka kwenye korodani ziazoanza kuzeeka..Ikumbukwe ya
kwamba kichocheo hiki testosteron hutengenezwa katika korodani.
Kichochezi cha testosteron ndicho kichochezi kikuu cha kiume
kinachowezesha tabia za kimwili za kiume.
Nini hutokea?
Kuongezeka ukubwa wa matiti kwa wanaume hutokana
na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo unaojulikana kitaalamu kama,
estrogen-androgen balance na hivyo kusababisha estrogen kutolewa kwa
wingi ama kuongezeka kwa msisimko wa matiti kwa kiwango cha zaidi ya
kawaida kwa kichocheo aina ya estrogen kilicho kwenye mzunguko wa damu.
Kichocheo hiki husababisha chembechembe
zinazojulikana kama ductal epithelia kuongezeka kwa wingi, kurefuka na
kugawanyika, kuongezeka kwa chembechembe za mafuta na kuongezeka kwa
mfumo wa damu kwenye matiti hutengenezwa kutoka kwenye vichocheo vya
testosteron na androgen kwa kutumia kimeng’enyo kinachojulikana kama
aromatase.
Aina za tatizo hili
-Puffy nipples –Kuongezeka ukubwa wa chuchu za matiti kutokana na kuongezeka kwa tishu aina ya glandular.
Ni nani aliyeko hatarini?
Visababishi vya kukua kwa matiti kwa wanaume
-Pure glandular gynecomastia – Huonekana zaidi kwa wale
wanaofanya mazoezi ya kujenga mwili, kutokana na matumizi ya dawa za
kujenga mwili ambazo zinakuwa na kiwango kikubwa cha kichocheo aina ya
testerone, ambacho hubadilishwa kuwa estrogen.
Kwa wanaume wembamba, tatizo hili hutokea kutokana
na kuongezeka kwa tishu za tezi za maziwa (breast tissue gland) pamoja
na kuwepo/kutokuwepo kwa tishu aina ya adipose.
Ni nani aliyeko hatarini?
-Wanaume walio na umri zaidi ya miaka 50.
-Wenye uzito uliopitiliza
-Unywaji pombe kupindukia
-Magonjwa sugu ya figo au ya ini
-Kuwepo kwa historia ya tatizo hili katika familia.
Visababishi vya kukua kwa matiti kwa wanaume
-Pseudogynecomastia – Kuongezeka kwa tishu
zinazozunguka chuchu za matiti na huambatana na kuwepo kwa wingi wa
tishu aina ya adipose. Mazoezi na kula vyakula venye virutubisho sahihi
huondosha tatizo hili.
-Unilateral/asymetrical gynecomastia – Ni
kuongezeka kwa titi moja pekee au la upande mmoja wa mwili wa mwanamume
kutokana na sababu mbalimbali. Titi la upande wa pili huwa kwenye umbile
na saizi ya kawaida. Bilateral gynecomastia ni kuongezeka kwa matiti
yote mawili.
-Hypogonadism – Kutofanya kazi kwa korodani vizuri na kuwa ndogo. Hii husababishwa na magonjwa mbalimbali.
-Umri – Kuzeeka pia kumehusishwa kutokea kwa tatizo hili
kutokana na kutolewa kwa uchache kwa kichocheo cha testerone na
kuongezeka kwa juhudi za kutengeneza kwa wingi kwa kimeng’enyo aina ya
estradiol kutoka kwenye kichocheo aina ya testerone.
Pia, mabadiliko ya mfumo mzima wa vichocheo mwilini hasa kwa wale wenye uzito uliopitiliza.
-Uzito uliopitiliza – Watu wenye uzito
uliopitiliza hupatwa na tatizo hili kutokana na kuharibika kwa mfumo wa
vichocheo mwilini na hivyo kuongezeka kwa kichocheo aina ya estrogen
mwilini mwao na wakati huohuo kupungua kwa kichocheo kingine aina ya
testerone.
-Saratani – Baadhi ya saratani kama vile ya kwenye
korodani, tezi lililo juu ya figo, saratani ya tezi la kichwa, huharibu
mfumo mzima wa vichocheo mwilini hasa wa kuweka sawa vichocheo kati ya
uanaume na uanawake (male-female hormonal balance).
-Hyperthyroidism – Kukua kwa ukubwa wa tezi la koo na hivyo kutengeneza kwa wingi kichocheo aina ya thyroxine.
- Tatizo la figo kushindwa kufanya kazi - Nusu ya
wagonjwa wote wanaotibiwa tatizo la figo kushindwa kufanya kazi kwa
kutumia hemodialysis hupatwa na tatizo hili la kukuwa kwa matiti
kutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo mwilini.
-Matatizo ya Ini – Dawa za kutibu magonjwa ya
kwenye Ini kama kuoza kwa ini, ini kushindwa kufanya kazi husababisha
kutokea kwa tatizo hili kutokana na kukosekana kwa uwiano sawa wa mfumo
wa vichocheo mwilini.
-Utapiamlo, ukame – Utapiamlo, ukame au
kujikondesha husababisha kupungua kwa kichocheo aina ya testerone na
kuongezeka kwa kichocheo aina ya estrogen na hivyo kuharibu mfumo wa
vichocheo mwilini.
Hii hutokana na kukosekana kwa virutubisho sahihi
mwilini ambavyo vingi husaidia kurekebisha mfumo wa vichocheo mwilini na
hivyo kumuepusha mtu na magonjwa mbalimbali pamoja na tatizo hili.
-Madhara ya dawa za kurefusha maisha (ARVs) kwa wagonjwa wa Ukimwi.
-Utumiaji wa dawa za kulevya kama bangi/marijuana.
0 comments:
Post a Comment