Makadinali 19 wapya wa Kanisa Katoliki wametawazwa
leo katika sherehe iliyofanywa Vatikani - uteuzi wa kwanza kufanywa na
Papa Francis tangu kuchukua uongozi wa Kanisa Katoliki.
Papa mstaafu, Benedict wa kumi na sita, naye alihudhuria, akionekana kwenye ibada ya hadhara kwa mara ya kwanza tangu kustaafu.
Mwandishi wa BBC Vatikani anasema uteuzi wa makadinali aliofanya Papa Francis unaonesha amebadilisha dira kutoka Ulaya na kuelekea maeneo ambako Kanisa Katoliki lina nguvu, yaani Amerika Kusini na Kati na Afrika.
Na kadinali mwengine mpya ni mkuu wa Kanisa Katoliki la Uingereza na Wales, Askofu Vincent Nichol.
0 comments:
Post a Comment