Watu 200 wamehamishwa kutoka makwao kisiwani Java
Nchini Indonesia, baada ya milipuko miwili ya volkeno kuutikisa mlima wa
Kelud.
Mmajivu ya volkeno yamerushwa kutoka kilele cha
mlima humo na kusambaa eneo kubwa Mashariki mwa Java na ripoti zinasema
kuwa majivu ya volcan ya centimita tano yalianguka ardhini.
Viwanja
vikuu vya ndege mjini Surabaya, Solo na Jogyakarta vimefungwa kwa
sababu majivu hali yametanda angani na hivyo kusababisha hali ambayo
marubani wa ndege hawataweza kuona mbali na pia tishio la kuharibu
injini ya ndege.
0 comments:
Post a Comment