Sunday 2 February 2014

MAANDAMANO YAJERUHI KADHAA BAADA YA POLISI KUVAMIA MSIKITI

Filled under:



Kumetokea ghasia mjini Mombasa, Kenya, baada ya polisi kuvamia msikiti unaohusishwa na wanaharakati Waislamu wenye siasa kali.

Polisi walitumia moshi wa kutoza machozi na risasi za raba dhidi ya waandamanaji, na imeripotiwa kuwa watu kadha walijeruhiwa.

Mashekhe wawili ambao wakihubiri katika msikiti wa Masjid Mussa walipigwa risasi na kuuwawa katika miezi ya karibuni.

Polisi wa Kenya wameuhusisha msikiti huo na kuajiri wapiganaji wa kundi la wapiganaji Waislamu wa Somalia, Al Shabaab, ambalo mwaka jana lilishambulia jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi.

0 comments:

Post a Comment