Bilionea huyo ni Ally Awadh wa Kampuni ya Mafuta ya Lake
OilAdaiwa Kumfanyia Unyama Mfanyakazi Wake
Jumanne,
Februari 11, 2014
Mlalamikaji anayedaiwa kupigwa na mabaunsa wa mfanyabiashara
bilionea Ally Awadh (Lake Oil), ameamua “kujipima
uzito” dhidi ya bilionea Mtanzania, Ally Edha Awadh ambaye ni mmiliki wa
kampuni ya Lake Oil ya Mikocheni jijini Dar es Salaam inayoagiza,
kuuza na kusafirisha mafuta na biashara nyingine nyingi.Awadh anayetajwa kama
mmoja wa mabilionea vijana nchini, amefunguliwa mashitaka Polisi ya kumteka,
kumdhalilisha kinyume cha maumbile na kumpora mali mmoja wa wafanyakazi wake.
Uamuzi
wa Waziri Mkuu Pinda umekuja baada ya Jeshi la Polisi nchini, katika kile
kinachoonekana ni kumgwaya bilionea huyo, kupuuza kumsaidia mlalamikaji huyo
mwenye umri wa miaka 32. Kwa sababu za kiutu na za kitaaluma, jina la mlalamikaji
tunalihifadhi kwa sasa.
Hatua ya Pinda imetokana na barua ya mlalamikaji ya
Novemba 29, mwaka jana aliyomwandikia baada ya Jeshi la Polisi-kuanzia Kituo
cha Oysterbay, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na hata Makao Makuu, kupuuza
kumsaidia mlalamikaji ili aweze kutendewa haki.
Baada ya kuipata barua ya
mlalamikaji, Pinda alimwagiza msaidizi wake, Leila Mgonya, amwandikie barua
Katibu wa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kazi hiyo ilifanywa
Desemba 29, mwaka jana.
Katika barua hiyo ya Pinda iliyoandikwa kwa niaba yake
na Mgonya, inasema, “Miongoni mwa mambo aliyofanyiwa mlalamikaji na mwajiri
wake (Awadh) ni pamoja na kupigwa na kujeruhiwa mwili mzima kama picha
zilizoambatanishwa na barua ya mlalamikaji zinavyoonyesha, kudhalilisha pamoja
na kudhulumiwa mali zake kama inavyobainishwa katika barua ya mlalamikaji.
“Kwa
kuwa suala hili limejikita zaidi katika utendaji wa Jeshi la Polisi,
imeelekezwa kuwa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ishughulikie suala hili
kikamilifu kwa lengo la kumsaidia mlalamikaji kupata haki yake kwa mujibu wa
sheria na kuona kuwa haki inatendeka.
“Aidha, Mheshimiwa Waziri Mkuu angependa
kupata mrejesho kuhusu suala hili. Tafadhali mfikishie Mheshimiwa Waziri
maelekezo hayo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.”
Pamoja na maagizo hayo ya Waziri
Mkuu, JAMHURI imebaini kuwa hakuna hatua zozote za maana zilizokwishachukuliwa
dhidi ya Awadh na washirika wake.
Barua ya mlalamikaji kwa Waziri Mkuu
Mlalamikaji
katika barua yake kwa Waziri Mkuu, anaanza kwa kusema, “Mheshimiwa, jina langu
lipo hapo juu ni kijana wa Kihindi (Mtanzania) umri wangu ni miaka 32 mzaliwa wa
Tanga, nina mke na watoto.
“Mheshimiwa, nimesomea uhasibu na nimefuzu mwaka
2004 masomo yangu… na nikaajiriwa na Ally Edha Awadh katika kampuni yake
iitwayo Lake Oil Ltd Septemba, 2010 na kuwa Finance Manager (Meneja Fedha)
katika kampuni yake.
“Bila matarajio yangu, ilipofika Mei 2, 2013 mwajiriwa
mwenzangu aitwaye Ahmed alifika ofisini kwangu na kuniarifu ya kwamba naitwa na
Mkurugenzi Ally Edha, ilikuwa saa 11:30 za jioni Alhamisi na bila kusita
nikaongozana naye hadi kwa Ally Edha nikifahamu naitwa kwa ajili ya kazi
kiofisi.
“Nilishangaa nilipofika tu ofisini kwake akahitaji simu yangu,
nikampa mara akamuagiza stafu mwingine aitwe Fahim akafuate laptop yangu na vifunguo
ya gari yangu ofisini kwangu na ofisini kwake tulipobaki mimi, yeye na Ahmed.
Alianza kunitukana na kuniambia mimi ni mwizi nimemwibia dola milioni 10 za
Marekani (Sh bilioni 16).
Mara ilipoletwa laptop yangu na funguo za gari
akanichukua na kuniagiza nimfungulie e-mail yangu. Nilikataa na kumwambia hii
ni mail yangu binafsi na siyo ya ofisi yake, siwezi kufungua pana kazi za
wateja wangu wengine (mimi ni mhasibu wa wengi). Akanitishia kunipeleka Polisi,
nami nikamkubalia.
“Mheshimiwa, tukifuatana na wafanyakazi wake wengine,
Ahmed, Fahim, yeye na K.V Choudry, tulishuka chini na kuingizwa katika gari ya
Ahmed. Gari ikawashwa na mara akamuagiza dereva Ahmed lile gari tulilopanda
lipelekwe godown (ghala) ili abadilishe gari kwenda Polisi. Cha kushangaza
nikaamrishwa nishuke pale godown na kuingizwa ndani, pamoja na wale tuliofatana
nao. Nilishangaa kuwakuta wengine wawili (yeye Ally Awadh anadai ni mabaunsa
wake) wanaitwa Waitey na mwingine ni Abeid.
Mabaunsa waanza kumlawiti
“Mheshimiwa,
wakajumuika pamoja wakanivua nguo, wakanilawiti. Wakanipiga sana kwa kutumia
nondo, mikanda mizito, makonde ya nguvu na huku huyo mtumishi mwenzangu Ahmed
akiwa ameielekeza pistol (bastola) kichwani kwangu kwa kuniambia leo ni kifo
changu endapo nitakataa kuyakubali anayotaka bosi wake, yaani Ally.
“Mheshimiwa,
mateso haya yalikuwa zaidi ya masaa mbili na nusu (zaidi ya saa mbili na nusu)
nikilazimishwa nikubali kutoa kila kitu changu (assets) nimpatie yeye,
vinginevyo wataniua na wakanionesha picha za maiti wawili zilizokuwepo katika
simu ya baunsa wake akidai (Ally) angeniua kama hao, na kunifunga katika mfuko
wa plastiki na kunipeleka shambani kwake Soga kunizika.”
Mlalamikaji
anaendelea kumweleza Waziri Mkuu kwamba kutokana na mateso makali na vitisho
alivyopewa, alilazimika kukubaliana na maelekezo aliyopewa, yote hiyo ikiwa ni
mbinu ya kunusuru uhai wake.
Apigwa picha akiwa uchi
“Ndipo Ally Edha
akanipiga picha nikiwa uchi na kusema endapo nitaenda Polisi, yeye atazitoa
hizo picha kwenye mitandao ya intaneti kunidhalilisha. Hivyo nikapewa shati
langu nivae na kupelekwa ofisini kwake na kulazimishwa niandike kukubali kwamba
vitu vyangu vichukuliwe,” anasema.
Mlalamikaji
anayedaiwa kupigwa na mabaunsa wa mfanyabiashara bilionea Ally Awadh (Lake Oil) Kwa
mujibu wa mlalamikaji, mali zilizochukuliwa ni:
A: Nyumba yangu na mke wangu
iliyopo Nairobi, Kenya
B: Gari zangu mbili (i) Toyota IST T786 BZG (ii) Toyota
Fortuner T503 BQC
C: Bastola yangu 6mm niliyonunua Mzinga.
D: Fedha taslimu
dola 100,000 (Sh zaidi ya milioni 160)
E: Mkataba wangu wa nyumba na duka
(vyangu) vilivyoko Uhuru Heights
F: Ofa zangu tatu za viwanja Kigamboni
Asainishwa
kwa nguvu
“Ndipo nikasainishwa; na majira ya saa 3 za usiku wakanitia katika
gari aina ya Navara nyekundu mali ya kampuni –dereva akiwa Ahmed wakiwamo
mabaunsa wawili, Ally Edha, na mimi. Hadi nyumbani kwangu Upanga.
“Mheshimiwa,
inasikitisha kwa sababu mke wangu alipopiga simu nikiwa kwa Ally alinilazimisha
niongee na mke wangu kwa lugha ya Kiingereza, na siyo Kihindi. Alikuwa anapiga
kwa kutoamini kwa nini niongee Kiingereza badala ya Kihidi hadi simu ikaisha
pesa ndipo tulipofika tukamkuta yupo chini anangoja aletewe vocha na mlinzi.
“Wakanibadilisha
shati na kunivisha la Abeid (langu lilijaa damu). Wakamweka chini ya ulinzi mke
wangu. Tukapanda juu nyumbani hadi sitting room wakamnyang’anya simu na
kumkalisha chini.
Ally Edha akanilazimisha nimpeleke bedroom (chumba cha
kulala), ndiye akazichukua documents (nyaraka) zote na hizo pesa na mara
wakaingia Choudry, Sree Kumar na Ramana ambao wote ni wafanyakazi wake; na ni
Wahindi wakiwa na laptop na printer.
“Ghafla wakiwa na hizo laptop huyo
Choudry na Kumar wakaelekezwa kuandika maneno ya mkataba ambayo mimi na mke
wangu tukalazimishwa kuweka sahihi zetu kukubali kuzitoa mali zetu kwa huyo
jambazi Ally. Nakumbuka hata watoto wanalia kutaka maziwa nyumbani Ally Edha
alizuia wasipewe.”
Mlalamikaji anaendelea kusema kwamba akiwa na maumivu
makali, Ally Edha alitaka siku ya pili amtolee pesa katika akaunti yake iliyopo
katika Benki ya STANBIC, Tawi la Nyerere Road; na akasema angezifuata hizo
fedha siku ya Jumamosi.
“Alizijua hizo fedha kwa sababu ni akaunti
niliyoitumia kuweka pesa za mshahara. Mshahara wangu ulikuwa Sh. milioni 6 kwa
mwezi.
Kama hilo halikutosha, alikuta chumbani kwangu vitabu vitatu vya hundi
za akaunti ya pamoja na mke wangu; Standard Chartered (Nairobi, 2), Benki ya
Exim (3), Benki ya NBC, akatulazimisha tuzitie sahihi zetu- na tukafanya
hivyo.”
Mlalamikaji, mkewe waonywa watauawa
“Siku hiyo aliniambia mimi na mke
wangu kwamba kama angesikia tumemueleza mtu yeyote haya mambo, angetuua. Kweli
tukaogopa sana hadi siku ya tarehe 4, 2013 ndipo alipomtuma Sree Kumar kuja
kuchukua zile milioni 22 alizoagiza nizitoe katiba akaunti yangu ile siku ya
tarehe 2 Mei 2013. Nilimkabidhi Sree Kumar akampelekea Ally Awadh.
“Mheshimiwa,
nakumbuka namna tarehe 8 Mei, 2013 Choudry (Mfanyakazi wa Ally Awadh)
alinitumia meseji mbili kwa kutumia simu yake kwamba angependa aje nyumbani
waniletee pochi waliyochukua siku ya tukio nyumbani kwangu ambayo ni ya mke
wangu yenye kadi yake ya ATM na kopi ya leseni ya udereva. Nikawaambia
sitokutana nyumbani, tukapanga anikute Mtaa wa Morogoro/Jamhuri akaleta
akanikabidhi bila ya kunisalimu.”
Danadana za Polisi Oysterbay
“Mheshimiwa
Waziri Mkuu, siku ya Jumamosi tarehe 4 Mei 2013 nilipatiwa wakili aitwaye
Mwanganga. Nikamueleza, akaamua tukamuone RPC Kova (Kamanda wa Polisi Kanda
Maalumu Dar es Salaam).
Tulifika saa za mchana, nikamueleza na nilipotaka
kumwonyesha majeraha yangu alikataa na kusema kuangalia majeraha sio kazi yake
ila alipiga simu Oysterbay akatuagiza twende. Tukafuatana na wakili hadi
Oysterbay.
“Mheshimiwa, hiyo tarehe 4 Mei 2013 tulifika Oysterbay tukamuona
ofisa mmoja simfahamu jina ila sura namfahamu (wakili wangu anamfahamu).
Hakuonekana kujali sana, ndipo akatupeleka ofisi nyingine (wakili anaifahamu).
Hapo huyo askari akamuita mama mmoja polisi ndipo akatupeleka ofisi nyingine,
ofisa akamuagiza andike maelezo naye akanisikiliza na akanipeleka kwa ofisa
mwingine. Huyo ndiye aliandika maelezo yangu.
“Cha kushangaza huyo ofisa
alianza kusema ‘wewe tayari umetajwa kwenye kesi nyingie ya Lake Oil’, lakini
tukamwambia aandike maelezo yangu. Yeye alidai ‘pana Mhimdi mmoja, Mukesh
ambaye ni Internal Auditor (Mkaguzi wa Ndani) wa Lake Oil yupo ndani rumande
hapo, na wewe pia unapaswa uwekwe ndani’.
Lakini huyo ofisa na mwanasheria
wangu walitoka nje. Cha kunishangaza wakili akanimbia eti inatakiwa niweke
dhamana nikatibiwe ili Jumatatu nirudi au nipelekwe kutibiwa nirudishwe rumande.
Lakini wakili baadaye alinifahamisha wameyamaliza- kampatia Sh 100,000; hivyo
ningepaswa nimrejeshee hizo pesa.
“Hivyo statement (maelezo) iliandikwa na
nikapewa medical examination report yenye case file no. OB/RB/7853/2013 ya
tarehe 4 Mei, 2013. Ndipo nilipoenda Sinza Hospitali kwa matibabu.”
Woga
wamfanya akimbilie Zanzibar
Mlalamikaji anasema kutokana na woga wa ahadi za
mateso zaidi au kuuawa kama alivyoahidi Awadh, aliamua Mei 5 aende mafichoni
Zanzibar.
“Tarehe 6 Mei nilipigiwa simu na Mutafungwa aliyejitambalisha kwangu
kwamba yeye ni OCD wa Kinondoni akisema amesikitishwa kuisoma statement yangu
na angependa kukuona. Hivyo nikarejea Dar es Salaam na tarehe 7 Mei nikaenda na
kaka yangu na wakili wangu.
Tukamwona, akaagiza kwa ofisa mwingine wa CID
kumweleza hiyo kesi ni ya ukweli kwa hiyo wakamatwe wahusika mara moja na
kuniagiza nishirikiane naye.
“Baada ya siku mbili, yaani Mei 9, nikapigiwa
siku na Salum (CID Osysterbay) akanieleza yeye ndiye mpelelezi wa kesi yangu na
angependa kuniona. Tahere 12 Mei nilimuona Salum. Kwa sababu ya kuwa Zanzibar
ndiyo maana nilichelewa kumuona. Akanisikiliza na kusema angepeleleza hiyo kesi
na angeniita.
“Mheshimiwa, kila mara huyu Salum hakunipa msaada ipasavyo kwa
madai kwamba hajamuona Ally Edha. Nilishangaa sana sababu ofisi ya Ally Edha
ipo, wanaijua na iweje waseme hawamuoni? Baada ya muda, katikati ya Mwezi wa
Ramadhani, Salum aliniita na kuniambia mwenzake aitwae James angeweza
kunisaidia kuipata silaha yangu kutoka kwa Ally na nikamuona huyo James ambaye
aliahidi Ally Edha akirudi safari yake kwa asilimia 90 nitapata pistol
(bastola) yangu. Akasisitiza pia akimuona siku ya kwanza tu Ally angenipatia
hiyo bastola.”
Aombwa chochote akishasaidiwa
“Nakumbuka katikati ya Oktoba,
mwaka jana Salum alinipigia simu akasema James anauliza endapo akinisaidia
kuipata hiyo bastola mimi ningempa zawadi gani. Nikamjibu, ‘Nitampatia
anachotaka’ ilimradi nipate bastola na vitu vyangu.
“Mheshimiwa, Nashangaa
tangu wakati huo walipoanza kutaka chochote kwangu, hawajanipigia tena, wala
kunisaidia.
Nami nilishajiandaa kuwakamatisha kwa rushwa. Nikaendelea
kupata matatizo ya kujificha kwa kuamini Ally Edha ana mamlaka ndani ya Jeshi
la Polisi na anaweza kunifanyia chochote atakacho.
“Mheshimiwa, Nikashauriwa
niende kutoa taarifa Makao Makuu ya Polisi (wizarani). Hivyo tarehe 27 Novemba,
mwaka jana nilienda huko nikamuona Bwana Laizer ambaye ni Kamishna. Nikamueleza
na nikamuonesha vielelezo. Alisikitika sana na hapo alimuagiza RPC wa Kinondoni
ashughulikie hilo jambo na amueleze kwa kila kinachoendelea.
“Hadi leo tarehe
29 Novemba, nimeamua nikatumie barua hii na vielelezo vyangu ili unisaidie,
kwani polisi hawanisaidii tangu nifanyiwe unyama huu.
Najiuliza na kujiona
mkiwa kwa kuamini kwamba huyu Ally Adha Awadh yupo juu ya sheria? Iweje polisi
wamlinde tangu Mei 2013 hadi leo pasipo kukamatwa? Mheshimiwa Naomba msaada
wako.”
Barua hii ya mlalamikaji aliweza kupeleka nakala kwa Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Utawala Bora, Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa.
Kwa upande wake,
Awadh amegoma kuzungumza na JAMHURI. Mara kadhaa amepigiwa simu yake, lakini
amekataa kuzungumza hata pale simu ilipopokewa. Ametumiwa ujumbe kwa nyakati na
siku tofauti, lakini hadi tunakwenda mitamboni alikuwa hajajibu.
Ujumbe mmoja
ulisema, “Habari za kazi.
Hapa ni gazeti JAMHURI. Tuna habari za kesi ya
… dhidi yako. Tunaomba kujua kama hili suala unalijua kabla hatujaichapisha.
Tangu jana tunaomba utupatie majibu- bila mafanikio. Tumetekeleza wajibu wetu
kitaaluma kwa hiyo hatustahili lawama. Mhariri”.
CHANZO: Gazeti la
Jamhuri.
Updates
Maelezo ya Naibu Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri, Jackton
Manyerere.
Naibu
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri, Jackton Manyerere amesema hivi punde
kwamba kweli magazeti yao, yote yamenunuliwa asubuhi na mapema baada ya
kuchapisha habari hiyo. Akizungumza
na mtandao wa habari5.com, Manyerere amesema kuwa mmiliki wa Kampuni ya Lake
Oil, Ally Awadhi alimfanyia mfanyakazi wake vitendo visivyo vya kibinadamu
akimtuhumu kumuibia Sh10 milioni. Amesema
pia mlalamikaji huyo alilazimishwa kuuza viwanja vyake, na nyumba yake iliyoko
Nairobi pamoja na kumfanyia mambo mengine mabaya. Manyerere
amesema baada ya kuandika habari hiyo magazeti yote ya Jamhuri yamenunuliwa
yote kabla ya kuwafikia wateja wao wa kila siku. Kwa
lugha nyingine, magazeti hayo yamenunuliwa na mtu mmoja kwa lengo la kuthibiti
habari hiyo isisomwe na watu wengi. Kutokana na kuwapo kwa malalamiko hayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda
aliagiza suala hilo lifanyiwe kazi.
CHANZO:CHADEMA DIASPORA
0 comments:
Post a Comment