Wazazi wengi hawana habari kuhusu hatari
zinazowakabili watoto wao wanapotumia vifaa vya tablets na simu za
mkononi almaarufu kama smartphones.Hii ni kwa mujibu wa utafiti
uliofanywa na BBC.
Takriban mmoja kati ya watoto watano walisema
kwamba waliwahi kuona kitu kwenye vifaa hivyo ambacho kiliwafadhaisha
kwa kiasi maradufu zaidi ya jinsi wazazi wao walivyodhania.
Utafiti mwingine umeonyesha kwamba
wazazi wapatao zaidi ya 20% hawaangalii kwa karibu yale ambayo watoto
wao hufanya kwenye mtandao.
Utafiti huo ulitumika ikiwa sehemu ya siku ya kuadhimisha Usalama wa Matumizi ya Mtandao.
Huku 90% ya wazazi waliohojiwa na BBC huko
Uingereza wakisema kuwa wamewahi kuwatahadharisha watoto wao kuhusu
usalama kwenye mtandao wanapotumia simu zao, wengi walisema kwamba wao
huwaruhusu watoto wao kutumia vifaa hivyo bila usimamizi wowote.
Vizuizi vya wazazi
"Cha kusikitisha ni kwamba hamna yeyote kati
yetu wa umri wowote ambaye hawezi kupata matatizo kwenye mtandao,"
alisema Tonny Neate ambaye ni mkuu wa shirika la Get Safe Online.
Bila kutumia vizuizi mbali mbali vya usalama na kibinafsi watoto huenda wakakumbana na mambo ambayo hayafai kwa umri wao ama umri wowote.
Bila kutumia vizuizi mbali mbali vya usalama na kibinafsi watoto huenda wakakumbana na mambo ambayo hayafai kwa umri wao ama umri wowote.
Usalama wa matumizi ya mtandao katika familia.
Utafiti huo pia ulionyesha kuwa watoto kati ya
umri wa miaka 13-16 wamo katika hatari zaidi za ukatili kwenye mtandao
wakilinganishwa na wale wa umri wa miaka 8-12. Hata hivyo wazazi hawana
hofu ikiwa watoto wao waliozidi umri huo kutumia vifaa vya tablet.
David Emm,ambaye ni mtafiti wa usalama katika maabara ya Kaspersky alisema kwamba:
''siku hizi wazazi hawana habari kuhusu hatari
za kutumia mtandao kwenye tablets na simu za mkononi kama walivyokuwa
hapo awali mtoto alipotumia tarakilishi.
"Watoto wanapotumia rununu na vifaa vyake kuingia kwenye mtandao hutumia mtandao ule ule wenye hatari, alisema.
"Wengi wanadhani kwamba rununu na zile tablets
hazihitaji kiwango sawa cha kinga kama tarakilishi. Lakini kadri
asilimia kubwa ya wazazi ambao hawachunguzi kile ambacho watoto wao
hufanya kwenye mtandao, mkondo huo wa mawazo unapaswa kugeuka."
Simu za kampuni ya Apple kama iPhone na tabiti
za ipad tayari zina vizuizi ambavyo mzazi anaweza weka ili mtoto
asiwezie kutumia.
Ni muhimu kuzifunga tandawazi kabisa au kutia umri mwafaka wa watu wanaoruhusiwa kutumia maudhui yaliyomo.
Kuna uwezekano wa kuwa na akaunti zenye vizuizi kwenye simu za Android na tablets.
Vidokezo kwa Wazazi.
Zaidi ya 50% ya wazazi walioshiriki utafiti huo
wa BBC walikuwa wameweka vizuizi kwenye simu zao lakini 40% pekee ya
wazazi hao walisema kuwa wamefanya hivyo kwenye simu za watoto wao pia.
Katika utafiti uliofanywa kwenye maabara ya
Kaspersky, 18% a wazazi waliwahi poteza fedha au data kutoka kwa simu
zao au tablets kwa sababu watoto wao walikuwa wakitumia vifaa vya wazazi
bila ya kuandaliwa kwa karibu.
Watoto walio huru sana kutumia sana mtandao hununua programu za michezo kwenye internet au Apps, na hivyo kutumia pesa vibaya.
Kamapuni ya Apple hivi karibuni iliambiwa
iwarejeshee wazazi kima cha dola milioni 32.5 ambao watoto wao
walinunua programu hizo bila ya idhini ya wazazi.
Watu wazima pia wanaonywa kuhusu usalama wao
kwenye mtandao wakati kampuni ya Microsoft ilipozindua utafiti wake wa
kila mwaka kuhusu usalama wa watu kwenye mitandao.
0 comments:
Post a Comment