WAFANYA
Biashara wa soko la Nyandira, wanaandaa maandamano wakidai
yatakoyoongozwa na Diwani wa Kata, Ruanda Zengwe (CHADEMA), yenye nia ya
kumtoa ofisini Mhandisi wa Wilaya, William Lameck, akatengeneza
barabara, inayowagharimu Mil.9.6/- kwa mwaka.
Kero
ya barabara hiyo, pia inaungwa mkono na wananchi wa Kata ya Nyandira,
ambao kimsingi wamedai watakuwa tayari kumuunga mkono Diwani na wafanya
biashara hao, ili kushinikiza Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na
Viongozi, kutengeneza barabara hiyo yenye adha kwao.
Alipohojiwa
na Gazeti hili jana kuthibitisha kama malalamiko ya wafanya biashara
hao ni ya kweli. na kama yupo tayari kuwaunga mkono kuongoza maandamano
hayo, Diwani Zengwe alisema kwamba,
“Madai
ya Wafanya biashara hao ni ya kweli, kila mwezi wanakatwa Ushuru,
Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ikiwa inachukua Sh. Laki 8/- kwa mwezi
ambapo kwa mwaka ni Mil.9.6/-; hivyo inasikitisha kwa nini barabara hiyo
haitengenezwi, kiasi cha kuhatarisha maisha yao.
“Mara
maandalizi hayo yatakapoiva, kama Diwani ninayejua uhalisia wa madai ya
wafanya biashara hao, jinsi wanavyoporwa fedha zao, halafu
hawatengenezewi miundo mbinu yao. ‘Nitakuwa tayari na nitaongoza
maandamano hayo’,kama yatakavyokusudiwa”.alisema Zengwe.
Pia
Zengwe alisema, anafahamu lipo fungu lililotengwa kwa ajili ya
ukarabati wa miundo mbinu ya barabara hiyo, lakini sielewi fedha hizo
zimeingia kwenye Tumbo na Mfuko wa nani! Kiasi cha kuacha wajawazito na
wagonjwa wakiwemo watoto wadogo, maisha yao yawe hatarini.
Aidha
kwa upande wake Mhandisi wa Wilaya ya Mvomero Lamecck alipoulizwa
alikiri kwamba, “Ipo asilimia 10% ya fedha za ukarabati wa barabara
hiyo, hivyo ni vizuri umuulize Diwani wa Nyandira, Zengwe, anafahamu
suala hili”, jambo ambalo limepingwa ikihofiwa fedha hizo zinatafunwa.
0 comments:
Post a Comment