CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimebaini hujuma
zinazodaiwa kufanywa kwa ubia kati ya Jeshi la Polisi na Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kutaka kuanzisha vurugu kwenye kampeni za uchaguzi mdogo
wa madiwani unaotarajiwa kufanyika kesho kutwa katika kata 26 nchini.
Chama hicho kimeeleza kuwa hata matukio ya kuvamiwa, kupigwa na kisha
kukamatwa kwa wafuasi wa CHADEMA ni matokeo ya hujuma hizo.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa
Oganaizesheni na Usimamizi wa Kanda, Benson Kigaila, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuelezea ushiriki na mkakati wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa.
Oganaizesheni na Usimamizi wa Kanda, Benson Kigaila, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuelezea ushiriki na mkakati wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa.
Mbali na kuelezea mkakati wa ushindi katika Jimbo la Kalenga, pia
Kigaila alielezea matukio yanayotokea katika kampeni ya uchaguzi mdogo
wa madiwani kwa kata 26 unaoendelea sasa sehemu mbalimbali nchini.
Akizungumzia ushirikiano wa Polisi na CCM katika kuihujumu CHADEMA,
Kigaila alisema mkakati huo ulianza wakati wa M4C Operesheni Pamoja
Daima, ambapo wakiwa mkoani Mbeya katika Wilaya ya Mbarali, waligundua
kambi ya vijana wa CCM wapatao 300 waliopangwa kufanya vurugu kwenye
mkutano wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, mkoani humo.
“Tulipobaini mbinu zao niliwasiliana na RPC Mbeya, chakushangaza
badala ya kushughulika na wahalifu hao, akaamua kumuita mwenyekiti wa
CCM wa mkoa huo na kumueleza wasitishe vurugu walizopanga kuzifanya na
kama zingefanyika, tuliwaambia tutamkamata mwenyekiti wa mkoa badala ya
wafanya vurugu na kweli wakasitisha,” alisema Kigaila.
Alisema kinachosikitisha ni kuona wafuasi wa CHADEMA wakipigwa na
kuumizwa, lakini polisi inawakamata watu walioumizwa badala ya
kuwatafuta waliosababisha maumivu hayo.
“Waliofanya fujo CCM, walioumizwa CHADEMA, waliokamatwa CHADEMA,
inakuwaje hali hii na haya mambo ya CCM kwanini yanaibuka kila
panapokuwa na uchaguzi?” alihoji Kigaila.
Alisema tayari malalamiko yao dhidi ya polisi wameyafikisha kwa
Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye ndiye mlezi wa vyama nchini na
kumuomba aingilie kati hali hiyo kabla uvumilivu haujawashinda wafuasi
wao.
16 wajitokeza Kalenga
Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi wa Jimbo la Kalenga lililoachwa
wazi na marehemu William Mgimwa, Kigaila alisema kazi ya kuchukua fomu
ndani ya chama imeshaanza na hadi jana watu 16 walishachukua fomu kuomba
ridhaa ya chama.
Alisema fomu za CHADEMA zimeanza kutolewa juzi na mwisho ni Februari 9 na hadi jana watu 16 walishachukua fomu.
Aliongeza kuwa fomu zinapatikana katika tovuti ya CHADEMA ya www.chadema.or.tz, pia makao makuu ya chama hicho pamoja na ofisi ya Jimbo la Kalenga.
Kigaila alisema Kamati Kuu ya CHADEMA itakutana Februari 12 kwa ajili
ya uteuzi wa mwisho wa mtu atakayepeperusha bendera ya CHADEMA.
Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga unafanyika kuziba nafasi ya
marehemu William Mgimwa aliyefariki dunia Januari Mosi nchini Afrika
Kusini alikokuwa akipata matibabu.
0 comments:
Post a Comment