CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kimemteua mwanasheria Sinkala Mwenda kugombea ubunge wa
Kalenga baada ya kuwashinda wenzake 13. Katika kinyang’anyiro cha uteuzi
huo kada aliyekimbia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kushindwa kura za maoni
mwaka 2010, Zubery Mwachura, aliambulia kura sifuri. Mwenda alitangazwa kuwa
mshindi baada ya uchaguzi uliofanyika juzi kwa zaidi
ya saa 10 mjini Iringa. Uchaguzi huo ulisimamiwa
na wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA taifa, Chiku Abwao
na Benison Kigaila, ambapo kura 132 zilipitisha jina la
mwanasheria huyo huku kura 122 zikimchagua Grace Tendega.
Katika uchaguzi huo, kada wa
CHADEMA na muuza magazeti maarufu mjini Iringa,
Aidan Pungili, aliambulia kura 2 wakati Daniel Luvanga
akipata kura moja. Wagombea wengine walioonyesha
kufanya vema baada ya kujiunga na CHADEMA wakitokea CCM ni
Dk. Evaristo Mtitu, aliyepata kura 32 na Ancent Sambala
aliyepata kura 22. Mgombea, Akbar Sanga, alipata kura
21; Rehema Makoga kura nne, Henry Kavina kura tisa, Mussa Mdede kura 48;
Mchungaji Samweli Nyakunga kura mbili na Mwalimu Vitus Lawa akipata kura
14. Kigaila
aliwataka viongozi wa CHADEMA Jimbo la
Kalenga kukijenga zaidi chama hicho na kwamba, baada
ya kampeni kuanza Wana CHADEMA wilaya zote za Mkoa wa
Iringa wataingia kazini katika jimbo hilo.
0 comments:
Post a Comment