Matukio ya unyama na ukatili ya kuwamwagia watu tindikali yameendelea kuikumba nchi.
Safari hii ni Imamu wa Jumuiya ya Sawiyatu Qadiria ambaye ni mkazi wa Tindiga eneo la Unga Ltd,jijini Arusha, Hassan Bashir (33), ambaye amemwagiwa kimiminika kinachosadikiwa kuwa tindikali sehemu ya mabegani iliyosambaa maeneo ya mgongoni na shavu la kushoto.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 3:45 usiku maeneo ya msitiki huo.
Hata hivyo, Sabas alisema upelelezi kuhusiana na tukio hilo bado unaendelea ikiwa ni pamoja na kutumia kopo lililokuwa na kimiminika hicho ambacho kimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kujua uhalisia wake.
Alisema, uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kwamba muda si mrefu kabla ya tukio hilo, Hassan, alikuwa anatokea maeneo ya kituo kikuu cha mabasi cha Arusha baada ya kuachana na wenzake wawili ambao walikuwa wanajadili kikao cha Maulid.
Alisema muda huo wa saa 3:45 alikuwa maeneo ya karibu na kwake Unga Ltd, ndipo alipomuona mtu amesimama kwenye kiambaza cha msikiti, alimsalimia, lakini hakumbuki kama alijibiwa.
Alisema wakati akiendelea kuelekea kwake, alihisi kuna mtu anamfuata na alipogeuka ili ajue ni nani, ghafla mtu huyo alimwagia kimiminika kinachosadikiwa kuwa ni tindikali.
Alisema mara baada ya kitendo hicho mtuhumiwa alikimbia na kuelekea kusikojulikana.
Alisema baada ya taarifa hiyo polisi waliokuwa doria maeneo ya karibu walikwenda katika eneo hilo na kukuta kopo dogo ambalo linasadikiwa kuwa lilikuwa na kimiminika kinachosaidikiwa kuwa na tindikali.
IMAMU AZUNGUMZA
Akizungumza kwa maumivu makali katika wodi ya wanaume majeruhi ya Hospitali ya Mount Meru jana, Hassan, alisema tukio hilo lilitokea baada ya kumaliza mazungumzo ya kuandaa maulidi ya msikiti mdogo wa babu yake wa Jumuiya ya Sawiyatu Qadiria, uliopo mtaa wa Tindigani.
Anasema wamepanga kufanya maulidi hayo Februari 16, mwaka huu na aliwataja aliokuwa akizungumza nao kuwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ismail Olomi na Abdallah Sadila Kaduma ambaye ni mwenyekiti wa ujenzi wa msikiti huo.
Anasema baada ya mazungumzo hayo alianza kurejea kwake, na akapita eneo moja lenye maduka mawili moja likiwa linauza bidhaa za Kiislamu alikutana na mtu akiwa amesimama jirani akiwa amevaa koti lenye rangi nyeusi.
Alisema alimsailimia, lakini hakuweza kujua kama aliitikia au la, na yeye akaendelea na safari zake, lakini kumbe mtu huyo baadaye alimfuata kwa nyuma na alipogeuka kumwangalia alishtukia akimwagiwa kimiminika hicho.
Akizungumzia sababu hayo ya kutendewa hivyo, Hassan alisema itakuwa ni kutokana na mgogoro wa ujenzi wa msikiti huo.
“Sijagombana na mtu wala kurushiana maneno na mtu lakini tukio hili naweza kulihusisha na ugomvi wa kugombea msikiti huo kati yake na jamaa mmoja (jina linahifadhiwa) ambaye alikuwa ananitisha kwa maneno kuhusu msikiti huo.
“Nilimwambia huyo jamaa kwamba nipo tayari kufa, wakati fulani aliwahi kumpiga mwanafunzi wangu (jina linahidhiwa pia) na baada ya kushtakiwa, Mahakama ya Mwanzo ya Maromboso mwaka jana ilimfunga kifungo cha nje cha mwaka mmoja,” alisema.
Kwa mujibu wa Kamanda Sabas, mtu mmoja anahojiwa na polisi kuhusiana na tukio hilo.
MATUKIO YA TINDIKALI
Kwa kipindi cha miaka mitatu tangu mwaka 2012, viongozi mbalimbali wa dini na wasichana wawili raia wa Uingereza wamemwagiwa tindikali kwa nyakati tofauti na watu wasiojulikana.
Viongozi hao na miezi waliyokutwa na matukio hayo ni Novemba mwaka 2012, Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga, Mei, mwaka 2013, Sheha wa Tumondo Mohamed Omary Said, Julai mwaka 2013, Shekhe Mkuu Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba.
Agosti 7, 2013, wafanyakazi wa kujitolea kutoka Uingereza, Katie Gee na Kirstie Trup, walimwagiwa tindikali wakiwa eneo la Mji Mkongwe mjini Zanzibar.

Septemba, 2013, Padri wa Parokia ya Machui ya Kanisa Katoliki Zanzibar, Anselem Mwang’amba.
0 comments:
Post a Comment