Mahakama ya Mwanzo ya Mtindiro wilayani Muheza mkoani Tanga,
imemhukumu kifungo cha miaka miwili jela Victoria Komba kwa kosa la
kujisaidia ndani ya kisimani na kuchafua maji pamoja na kuwatusi
wanakijiji.
Hata hivyo hukumu imetolewa wakati mshitakiwa ametoroka na hajulikani alipo.
Komba mkazi wa kijiji cha Kwabota alihukumiwa na Hakimu Mkuu
Mwandamizi Kisimbo Aza na kudaiwa mahakamani hapo kuwa Januari 27 mwaka
huu wanakijiji cha Kwabota walikubaliana kuchimba kisima kutokana na
shida ya maji.
Alisema mtuhumiwa huyo alikataa kushirikiana na wenzake na kutamba
kuwa hata kama hakuchimba atachota maji kwa nguvu na wakikataa
atafanya jambo baya.
Alisema siku iliyofuata mfungwa huyo mtarajiwa alikwenda kisimani akajisaidia kisha kuondoka.
Mahakama iliambiwa kuwa baada ya mtuhumiwa kwenda haja wanavijiji
bila kujua walichota maji hadi yakabakia kidogo na walipendelea
kuchota mwananchi mmoja alipandisha kinyesi cha binadamu ndani ya chombo
kilichokuwa kinatumiwa.
Komba alikamatwa na kufunguliwa mashtaka mawili ya kuchafua maji
na kinyesi na kuwatukana wananchi, hata hivyo ilielezwa kuwa wakati
anapelekwa rumande baada ya kukosa dhamana mshitakiwa huyo alimtoroka
mgambo wa mwanamke walipofika stendi kuu ya mabasi wilayani Muheza.
Walikuwa wanaelekea kwenye mahabusu gereza la Maweni mjini Tanga, hata hivyo hukumu hiyo itaanza kutekelezwa atakapokamatwa.
0 comments:
Post a Comment