MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Baby Madaha kwa wiki moja sasa amekuwa akimsaka Mkurugenzi wa kampuni ya 5 Effects, William Mtitu ili amkabidhi ‘muvi’ yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘The Gal Bladder’ ili amsambazie.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Madaha alisema kuwa, amekuwa akifika katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Magomeni Usalama ili kuonana naye lakini anaambiwa yupo katika harakati za kushughulikia kusambaza filamu yake ya ‘Big Deal’
inayozungumzia uingizwaji na madhara ya dawa za kulevya nchini.
“Nimepata taarifa kuwa, wasanii wengi wameanza kupeleka muvi zao kwake ili awasambazie, ndiyo nami niliona nimfuate, kwani nasita kupeleka kwa wahindi kwa sababu wanapunja katika suala la malipo, lakini kila nikienda ofisi kwake simkuti,” alisema Madaha.
Madaha alisema kuwa, licha ya yeye kuwa miongoni wa wasanii waliocheza kwa ufasaha filamu ya Big Deal baada ya kuombwa na Mtitu, imekuwa ni ajabu kwake kumsaka kiasi hicho, kwani hata simu yake ya mkononi akipiga muda mwingi inakuwa inatumika.
“Muda mwingi naumiza kichwa namna ya kumpata Mtitu, kwani nilikuwa naye wakati wa kurekodi filamu yake itwayo Big Deal, lakini baada ya hapo nashindwa kujua kwa nini imekuwa hivyo, kwani hata nikienda ofisini naambiwa katoka, nikipiga simu inakuwa inatumika,” alisema Madaha.
0 comments:
Post a Comment