Kuporomoka kwa jengo la
ghorofa Mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar es Salaam Machi 29 mwaka huu na
kusababisha vifo vya zaidi ya watu 36, kunadaiwa kutokana na uzembe wa
serikali.
Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti
iliyotolewa Novemba 24 mwaka huu na taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza,
asilimia 87 ya watu waliohojiwa, iliitupia lawama serikali kwamba inahusika kwa
kiasi kikubwa.
Asilimia 47 ya watu
waliotoa maoni yao juu ya kuanguka kwa jengo hilo, ilisema kuwa uzembe wa
wakaguzi wa majengo wa serikali pia ni miongoni mwa chanzo kingine.
Pia ripoti hiyo inaeleza kuwa
asilimia 32 ya waliohojiwa walisema kuporomoka kwa jengo hilo kulisababishwa na
kampuni ya ujenzi iliyokuwa ikishikilia dhamana ya ujenzi wake.
Aidha, ripoti hiyo ambayo imejikita
katika mahojiano ya watu 333 katika wilaya zote tatu za Dar es Salaam,
inaonyesha kuwa asilimia 18 ya maoni yaliyotolewa kuhusu sababu za kuporomoka
kwa jengo hilo ni uzembe wa manispaa husika.
Mbali ya hayo, ripoti hiyo inaeleza
kuwa asilimia 57 hawafahamu chochote kama kuna fidia zilizokuwa zimelipwa
kwa waathirika ama familia zao.
Ripoti hiyo ya utafiti ilikwenda
mbali zaidi na kubainisha kuwa maoni juu ya suala la mgawanyo wa wajibu ni
sehemu kubwa ya jukumu, ambapo asilimia 46 ilisema wahusika
hawafanyi kazi kwa kuhakikisha kuwa sheria za ujenzi zinafuatwa badala
yake imekuwa ni kinyume.
Asilima 32 ya waliohojiwa pia
waliitupia lawama kampuni ya ujenzi kwa ajali mbaya wakati ni suala la wajibu
binafsi, lakini pia asilimia 78 walikubaliana kwamba rushwa ni chanzo cha
majanga kama hayo.
0 comments:
Post a Comment