Mwenyekiti wa klabu ya Simba ,Ismail Aden Rage amemwandikia
rasmi barua Raisi wa shirikisho la soka Tanzania (TFF),JAMALI MALINZA akilitaka
shirikisho hiloo kupitia upya maamuzi yake kumtaka aiitishe mkutano mkuu wa
dharura wa wanachama ndani ya siku 14.
Rage amechukua hatua hiyo siku moja baada ya kuwaeleza
waandisha wa habari kuwa hatatekeza maagizo hayo ya kamati ya utendaji ya TFF
kwani kwa mtazamo wake,alifikiri kuwa wangekemea kile kilichoitwa mapindinduzi yaliyofanyka na kamati ya utendaji ya simba
Jumamosi iliyopita ,Raisi Malinzi aliwaambia waandishi wa
habari kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya Kubaini mgogoro ndani ya Simba kwani
wamepokea barua mbili,moja kutoka kwa kamati ya utendaji ikieleza kumsimamisha
Rage na nyingine ikieleza kutotambua uamuzi huo.
Rage alisema amesikitishwa na uamuzi wa TFF kutokana na
maagizo hayo kwa mtazamo wake,alifikiri watakemea vitendo hivyo vya kufanya
mapinduzi na si vinginevyo.
Rage alisema”siwezi kuitisha mkutano kwa sababu kufanya
hivyo ni sawa na kupokonywa madaraka yangu tena mbaya zaidi napangiwa hadi
ajenda ya kuzungumza ,na endapo TFF watanilazimisha kufanya hinyo nitajiuzulu”
Hata hivyo,jana Rage
muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda nchini Dubai na Uingeleza kwa
shughuli za kikazi za ubunge inakadiriwa
kuwa amemwandikia barua Malinzi akimtaka wapitie upya maamuzi kwa sababu
kilichofanywa na kamati ya utendaji ya simba ni kunyume na katiba ya simba ,TFFna
FIFA
Aliongea akisema hata kwa mujibu wa katiba ya nchi,Raisi anaposafiri
na makamu wa Raisi kukaimu nafasi hiyo,hana mamlaka ya kuvunja baraza la mawaziri
wala kuteua mtu,iweje leo kaimu mwenyekiti wa simba wae na mamlaka hayo?
Kwa mujibu wa Rage katiba za TFF ambazo zinatokana na katiba
ya FIFA zilishapiga marufuku mapinduzi ya uongozi wa soka,hivyo basi
kilichofanywa na kamati tendaji ya simba ni kwenda kinyume na katiba ya FIFA
Mwenyekiti huyo alisema kimsingi Kamati ya utendaji ya TFF inapaswa
kulipeleka suala hilo katika kamati ya sheria kwa mwongozo
Bwana Rage amesema ‘’ni imani yangu raisi wa TFF,bwana Malinzi
takubaliana namI na kupitia upya maamuzi ya KAMATI TENDAJI kwani kilichofanyika
ni kinyume na katiba ya Simba na TFF
KAMATI TENDAJI
ilitatangaza kumsimamisha rage wakati akiwa hayupo nchini na kumkaimisha
kaimu makamu mwenyekiti Joseph Itangare na kitaarifu TFFambayo ilipinga
mapinduzi hayo,ili ikampa rage siku 14 kuitisha mkutano ili kumaliza mgogoro
huo ndani ya simba
0 comments:
Post a Comment