Kutokana na hatua iliyochukuliwa na Chama cha
Democrasia na Maendeleo Chadema dhidi ya
aliyekuwa Naibu waziri wake ,Zitto kabwe
na mjumbe wa zamani wa kamati kuu,DKt
kitila Mkumbo,haitofautiani sana na iliyowahi kuchukuliwa kwa katibu mkuu wa zamani,Dk Aman Kabourou na
makamu mwenyekiti wa zamani,Chacha wangwe.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Mkuu
wa Chama hicho Tundu Lissu wakati akijibu hoja zilizotolewa juzi na viongozi waliovuliwa nyadhifa kwa madai ya
kukichafua chama.
Tundu Lissu alikanusha madai ya Zitto kwamba alichukua hatua
kutokana na msimamo wake kuhusu kutochukua
posho za vikao na suala la Ukaguzi wa Ruzuku ya Vyama vya Siasa,akisema
kiini ni waraka wa siri waliouandaa dhidi ya uongozi wa juu wa Chadema,nasisitiza
kuwa hawa wamechukukuliwa hatua kutokana
na kukiuka maadili ya chama na mashitaka
yote 11 yanayowakabili na mengineyo yaliyomo kwenye waraka wa siri walouandaa.
Lisssu alisema hatua zilizochukuliwa
na kamati kuu(cc) ya chama hicho dhidi yao ni halali na si mara ya kwanza kwa viongozi wa chama hicho kuvuliwa nyadhifa
kwa kuwa ilifanyka dhidi ya Kabourou mwaka 2004 na Chacha Wangwe mwaka 2007.
Lissu alisema wakati
bwana Kabourou alipovuliwa madaraka zito alikuwa mjumbe wa kamati
kuu,sasa kama kamati kuu mwaka 2004 na 2007 ilikuwa sahii kwa nini mwaka 2013
isiwe sahii Lissu alihoji.
Kabourou hivi sasa yuko CCM
kuhusu hali ya chama hicho kutokana na mgogoro huo,Lissu alifafanua kuwa
CHADEMA imestahimili mambo makubwa yakiwamo ya wangwe na zitto
kuhusu mkakati
ulioandaliwa alisema ni wa makusudi kwa kuwa chama kilishatangaza mwaka jana
mwongozo kwa wanachama wanaotaka kugombea uongozi yakiwamo masharti ya wahusika
kuwa wazi nakutotumia fursa hiyo kukashifiana ‘’kama waraka huo uliomkashifu
Mwenyekiti Freeman Mbowe.
"waraka huu umetoa matusi dhidi
ya mwenyekiti wetu,ikiwamo kuitwa ana elimu ya chini na hana akili ndogo na
nzito halafu mtu huyohuyo aliyetoa matusi anasema anakuheshimu chama.
Kuhusu suala ka ruzuku,Lissu
alieleza kuwa chama hicho kumefuata taratibu zote kama vyama vingine vyilivyo kaguliwa,isipokuwa ofisi ya mdhibiti
na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikal(CAG) Iliyolazimisha vyama vya siasa kujikagua kwa fedha
zao,wakati kazi hiyo ni yake kwa mujibu wa sheria.
Lissu alisema zitto akianzisha
hoja ya ukaguzi wa hesabu za vyama na kuvishutumu kuwa havijakaguliwa,msajili
wa vyama vya siasa ndugu Fransis Mutungi
Alishamwandikia barua CAG ya kumtaka kufanya kazi yake ya ukaguzi kwa mujibu wa
sheria
‘’sasa kinachoshangaza anayosema
sisi tulisha yafanyia kazi na nyaraka zipo,tatizo lake hakanyagi hapa ofisini
haya atayajuaje?lakini pia kuhusu kujiondoa kwenye saini ya kuchukua fedha
,hilo nalo si kweli,kwani hakuwahi kuwa mmoja
wa wanaosaini sasa atajiondoaje
?alihoji
Alisema alichofanya zitto kuhusu
suala la hesabu za serikali ni kutumia fursa kuchafua chama ,siku 14 mapema
,mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa chama chadema ,john mniyika alisema
hatma ya viongozo hao waliovuliwa madaraka itajulikana baada ya siku
14,watakapowasilisha utetezi wao kwa chama hicho
Hali hio inatokana na uamuzi wa
sekretariati ya chama hicho iliyokuta an juzi,kubariki uamuzi wa CC ya chama
kuwavua nafasi zote za uongozi,mbunge huyo na mwenzake ,kwa kuwaandikia rasmi
barua ya mashitaka yenye makosa 11 kwa kila mmjoja
Sekretarieti hiyo ilipitia uamuzi
huo na kuridhia barua hizo za mashitaka na kutoa siku 14 kwa watuhumiwa
kujiteetea kwa maamdishi,myika alisema pamoja na barua ambazo wanatarajia
kukabidhi leo,pia watuhumiwa hao watapewa fursa ya kujitetea mbeleya cc
Aidha ,alitetea uamuzi wa CC ya chama hicho wa
kuwachukulia hatua Zitto na Kitila kuwa
ulifuata taratibu na kanuni zote za chama hicho na ulikuwa wa haki,alisema kwa
mujibu wa kanuni za chama hicho ibara ya 5.4cc bila kuathiri katiba ,inaweza
kumvua madaraka wakati wowote mwanchama,pale itakapo thibitika kwenda na utaratibu wa chama
Aidha alisema ibara ya 6.36
ambayo anaainisha mamlaka ya uwajibishwaji,inabainisha kuwa viongozi
waliochaguliwa na mkutano mkuu wanaweza kuvuliwa madaraka yao na mkutano
huo,lakini waliochaguliwa na baraza kuu kama Zitto na Dk Kitila CC inaweza
kuwavua wakibainika kwenya kinyume.
Mnyika alihadharisha juu ya waraka
uliosambazwa kwenyemitandao ya kijamii kuwa umeghushiwa na kuhaririwa na kwamba
waraka halisi wa chama hicho kinao na una madai na mikakati mizito dhidi ya
chama hicho hasa viongozi wetu wakuu.
Lissu aliongea pia nakusema mkutano wa Zitto na Dk kitila wa waandishi wa
habari haukujibu hoja yoyote zaidi ya kupindisha lengo
Alisema viongozi hao hawakuvuliwa madaraka yao
kutokana na sababu walizoainisha bali walichukuliwa hatua hiyokutokana na
kutaka kufanya mapinduzi.
0 comments:
Post a Comment