Tuesday, 26 November 2013

MWILI WA MWANAFUNZI ALIYEUAWA KENYA WAWASILI NCHINI

Filled under:






Mwili wa mwanafunzi mtanzania Jerry Issack Mruma (23) aliyeuwa Nairobi nchini Kenya umewasili nchini jana na kupokelewa  na ndugu na jamaa wna marafiki katika uwanja wa ndege wa kumataifa wa Mwalimu Juliasi Kamabalage Nyerere

Mwanafunzi huyo Jerry alikuwa akisoma katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani chenye tawi nchini Nairobi.mwanafunzi huyo(Jerry) aliuawa nchini Kenya mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mwili wa mwanafunzi huo  unatarajiwa kuzikwa leo katika makabuli ya kinondoni,ndugu,jamaa na marafiki wamejitokeza katika maziko ya kijana huyo yatayofanyika saa 7.oo mchana  katika makabuli ya kinondono

Marehemu ni mtoto wa aliyekuwa mhariri mtendaji wa Tanzania standard Newspapers(TSN), wachapishaji wa gazeti la Daily news,Sunday news,Habari leo
Jerry mbali na kuwa mwanafunzi ,pia alikuwa ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya kilimo jijini Nairobi,husussani inayoshughulikia masuala ya kilimo

Mwili wa jerry ambaye alikuwa akisoma shahada ya uzamili ya utawala wa biashara(MBA),ulipatikana mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kijana huyo kuripotiwa wakati akitoka katika hafla ya usiku wa mtanzania.

Taarifa ya awali iliyotolewa na chuo hicho kuhusu kutoweka kwa jerry tangu jumamaosi iliyopita,ilisema alikuwa akitafutwa,kabla ya mwili wake kukutwa baada ya msako mkali ulioongozwa na kaimu mkuu wa usalama wa chuo,police na wanajumuiya wa chuo hicho.

0 comments:

Post a Comment