Wafanyakazi raia wa Kenya wa mashirika ya misaada ya
kibinadamu ambao walikuwa wametekwa na wapinaji wa kiislamu wa Al
shabaab mwaka 2011 wameokolewa na majeshi ya Kenya.
Daniel Njuguna ambaye alikuwa akifanya kazi
katika shirika la Madaktari wasio na mipaka Medecins Sans Frontieres MSF
na James Kiarie wa Shirika la Care International, walichunguzwa afya
zao na walitarajiwa kusafirishwa kwenda Nairobi.
Awali walikuwa chini ya uangalizi wa majeshi ya
Kenya ambalo lipo kwenye kikosi cha Umoja wa Afrika kilichopo nchini
Somalia AMISOM.
Kenya ilituma majeshi yake kwenda nchini Somalia
mwaka 2011 kujiunga na AMISOM kufuatia matukio ya utekaji nyara
yaliyokuwa yakiendeshwa na wapiganaji wa Al shabaab katika mipaka ya
nchi hiyo na Somalia.
Majeshi ya AMISOM yakishirikiana majeshi yale ya
serikali ya Somalia yamekuwa yakiendesha mapambano dhidi ya wapiganaji
wa Al Shabaab ambao wanafadhiliwa na kundi la kigaidi la al Qaeda
linaloshikilia maeneo ya kusini na katikati mwa Somalia.
0 comments:
Post a Comment