Mtoto mwenye umri wa miaka miwili nchini Uingereza
Riley Ward amepokea sifa kedekede kwa kuokoa maisha ya mamake kwa kupiga
nambari ya simu 999 baada ya mamake kuzimia.
Wahudumu wa afya katika kituo cha kupokea simu
za dharura nchini Uingereza walisema kuwa walipokea simu ya mtoto mdogo
aliyewambia ''Mama amelala''
Wahudumu hao walifanikiwa kwenda
nyumbani kwa mtoto huyo katika mtaa Leicestershire, na kumpa huduma ya
kwanza mamake mtoto huyo na kisha kumpeleka hospitalini.
Walimfanyia upasuaji wa dharura baada ya
kupatikana na damu iliyokuwa imeganda kichwani huku akivuja damu
nyingine kutoka katika kizazi chake.
Sasa mtoto huyo Riley Ward amezawadiwa kwa
kitendo chake cha ujasiri na wahudumu hao waliosema kuwa huyo ndiye
mtoto mchanga kabisa kuwahi kupiga simu kituoni humo.
Mamake , Dana Henry, alimtaja mwanawe kama shujaa wake mdogo.
Dana mwenye umri wa miaka 27 alisema kuwa alishtushwa sana na kitendo cha mtoto wake aliyekuwa na uwezo wa kupiga simu.
Pia alisema kuwa ameweza kuwafundisha watoto wake wadogo namna ya kupiga simu ya dharura ikiwa yeye na mumewe hawahisi vizuri.
0 comments:
Post a Comment