Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewafikisha mahakamani
Wahasibu Wasaidizi wawili wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kosa la
kuomba na kupokea rushwa ya Tshs (1,500,000/-) Milioni moja na laki tano
kutoka kwa mgonjwa.
Washitakiwa
hao ni Seka Ntiro (33) na Agrey Sigalla (35) ambao walisomewa mashitaka
yao Jumanne tarehe 25/02/2014 mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya
Kisutu jijini Dar-es-Salaam - Waliarwande Lema.
Mwendesha
mashitaka wa TAKUKURU Makao Makuu – Maghela Ndimbo alieleza mahakamani
hapo kuwa washitakiwa waliomba na kupokea hongo ya Tsh 1,500,000/=
kutoka kwa Magreth Mpande ili waweze kumsaidia asilipie gharama za
matibabu ya marehemu mama yake wakati amelazwa katika hospitali hiyo,
kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
Na. 11 ya Mwaka 2007.
0 comments:
Post a Comment