Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini (Chadema), Dk.
Wilbroad Slaa, amewaonya baadhi ya wanachama wanaochafuana kwenye chama
hicho waache mara moja vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Dk. Slaa amesema, kutangaza nia siyo
dhambi ni haki ya mwanachama bila kuwapo kwa migogoro ila anapaswa
afuate kanuni za chama.
Hata
hivyo, Dk. Slaa amekanusha kuwapo kwa mpasuko ndani ya chama Jimbo la
Songea mjini ambapo alisema yeye kama katibu mkuu bado hajapata
malalamiko rasmi ya wanachama kugombana ingawa amekemea wanachama
kuchafuana na kuzushiana uongo.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kanda Kusini, Matiko Matale, alipohojiwa
alisema kuwa taarifa ya Mwenyekiti wa Chama hicho mkoa kutangaza nia ya
kugombea ubunge jimbo la Songea mjini alipata ila hakufuata utaratibu na
wala hakupata baraka toka ndani ya chama.
Alisema
kwa sasa anajiandaa kuitisha kikao cha kamati ya utendaji cha kanda ili
kujadili mambo mbalimbali yakiwamo ya chaguzi kwani ametangaza nia
mapema.
Naye
mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chadema Taifa, Edson Mbogoro, amewaambia
waandishi wa habari kuwa kutangaza nia siyo dhambi ila yeye binafsi
anasubiri mchakato na taratibu za chama zinavyoagiza.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa chama hicho mkoa Joseph Fuime hakuweza
kupatikana kuzungumzia tuhuma hizo kwani kila alipopigiwa simu zake zote
za mkononi zilikuwa zimezimwa.
0 comments:
Post a Comment