Maafisa wanaosaidia katika harakati za kuitafuta
ndege ya Malaysia ya MH370 iliyopotea majuma tatu yaliyopita ,
wametangaza kuwa wanabadilisha eneo la kuitafuta mabaki ya ndege hiyo.
Eneo hilo jipya litakuwa kilomita elfu moja mia moja kazkazini mashariki mwa kusini mwa bahari hindi.
Mamlaka
ya usalama wa baharini nchini Australia imesema kuwa hatua hiyo
inatokana na taarifa muhimu na utafiti wa Malaysia pamoja na matokeo ya
utafiti wa rada ya ndege hiyo iliyotoweka.
Ndege hiyo iliyotoweka March tarehe 8 ikiwa na
abiria 239 sasa inadaiwa kwamba ilikuwa katika mwendo wa kasi kinyume na
ilivyokadiriwa na kwamba huenda iliishiwa na mafuta ghafla.
Meneja mkuu wa shirika la utafiti wa anga za juu
ya Australia John Young, amesema utafiti mpya unaonesha kuwa ndege hiyo
ya MH370 ilikwea juu na kufululiza kwa kasi mno na hiyo inaweza kuwa
sababu ya mafuta ya ndege hiyo kumalizika haraka.
Kutokana na hesabu hiyo mpya eneo la kutafutwa
kwa ndege hiyo imehamishwa hadi umbali wa kilomita 1,850 Magharibi mwa
Perth na itakuwa katika eneo lenye kilomita 319,000 mraba katika bahari
Hindi .
0 comments:
Post a Comment