Wakili wake aliyefahamika kwa jina moja la Jadeda alisema kwamba, mtu yeyote aliyerukwa na akili anaweza kupanga hatua kwa hatua kutekeleza mauaji kama alivyofanya mtuhumiwa na asijue kama kitendo alichokifanya ni kosa.
Wakili huyo alisema: “Wakati naongea naye kwa mara ya kwanza ilikuwa kama naongea na mti,” alisema Wakili Jadeda.
Wakili huyo alifafanua kuwa hali hiyo alikuwa nayo mtuhumiwa kwa kipindi cha wiki mbili au nne hivi.
Akaiambia mahakama iliyokuwa imefurika wasikilizaji kuwa inawezekana kabisa kuwa mtuhumiwa alifanya kosa hilo bila kujua kuwa alichokuwa akikifanya kilikuwa ni kosa na akili yake ilimuambia kuwa anachokifanya kinakubalika kisheria.
Wakili huyo mengi aliyokuwa akiyasema katika makahakama hiyo yalikuwa ni kupinga maoni ya upande wa mashtaka ambao ulikuwa ukisema na kusisitiza kuwa mtuhumiwa alikuwa akijua kitendo alichokuwa akifanya kwamba ni kosa kisheria.
Akisoma hukumu Mheshimiwa Jaji Makame alikubaliana na suala la mtuhumiwa kuwa na dhamira ovu (Malice aforethought), hasa kwa kuangalia vitendo vya mtuhumiwa tangu maandalizi, dhamira na akiwa na utambuzi kwamba, akiwanywesha wanawe sumu itawasababishia kifo.
Jaji alisema hiyo inadhihirisha kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua ni nini anachokifanya, na si lazima ajue kwamba kufanya hivyo ni kosa.
Jaji Makame alikuwa ameshawishika kuamini hivyo kutokana na barua nne alizoziandika mtuhumiwa kabla ya kutekeleza mauaji hayo, ambazo aliziandika sambamba na tendo alilofanya Februari 21, 1978.
Source:Global publisher
0 comments:
Post a Comment