Mahakama nchini Misri imewahukumu kifo watu 529
ambao wanasemekana kuwa wafuasi wa Rais aliyeng'olewa mamlakani Mohammed
Morsi.
Watu hao walikabiliwa ma mashitika mbali mbali yakiwemo mauaji ya polisi na kuwavamia polisi.
"Wafuasi hao wa chama kilichopigwa
marufuku, cha Muslim "
Brotherhood, ni sehemu ya kundi lengine kubwa la
watu zaidi ya 1,200 wanaoaminika kuwa wafuasi wa Morsi.
Maafisa wa utawala nchini Misri wamekuwa
wakiendesha msako mkubwa dhidi ya wafuasi wa vuguvugu hilo, tangu Morsi
kuondolewa mamlakani mwezi Julai mwaka jana.
Maelfu wamekamatwa huku mamia wakiuawa.
Mahakama hiyo ilitoa hukumu baada ya vikao
viwili pekee ambapo mawakili wa watuhumiwa walilalamika kuwa hawakupewa
muda wa kuwasilisha kesi yao vyema.
Mauaji wanayodaiwa kufanywa na watuhumiwa
yalitokea Kusini mwa Misri, mwezi Agosti, baada ya vikosi vya usalama
kuvunja kambi mbili za wafuasi wa Morsi waliokuwa wanataka arejeshwe
mamlakani.
0 comments:
Post a Comment