Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana
amesema hana mpango wa kuwahoji Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba
wanaotokana na chama hicho kwa sababu ya misimamo yao inayokinzana na
miongozo ya chama, kwa kuwa anawafahamu wote kwa majina na idadi yao
haizidi kumi.
Kauli hiyo ya Kinana inafuatia taarifa
zilizoripotiwa na gazeti hili hivi karibuni kuwa, CCM kimeanza kuwahoji
baadhi ya wabunge wake, ambao ni Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kwa
sababu ya kupingana na maelekezo ya chama hicho kuhusu Muundo wa
Serikali mbili.
“Sisi (CCM) hatuhoji mtu kwa sababu ya kuwa na
msimamo tofauti, kwani hawa wenye msimamo tofauti na chama hawazidi kumi
ama siyo zaidi ya 15,” alisema Kinana na kuongeza;
“Hawa watu mimi nawajua kwa majina, mmoja (jina
tunalo) ni hatari zaidi kwa sababu anaweza kuwakusanya wengine na
kuwashawishi wafuate msimamo wake, lakini waliobaki wote, hawatishi kwa
kuwa wanabaki na misimamo yao wenyewe.”
Kwa mujibu wa habari hiyo, wajumbe waliohojiwa ni
wale wanaotokana na Ubunge wa Jamhuri ya Muungano na ambao wanataka
Muundo wa Serikali tatu. “Ni kweli hata mimi niliitwa na akaniambia
(mwakilishi wa chama) ametumwa aniletee ujumbe kuwa niko kwenye orodha
ya watu 90 na nikiendelea na msimamo wangu nitachukuliwa hatua,”
alieleza mmoja wa wajumbe waliodai kuwa wamehojiwa na Mjumbe wa Kamati
Kuu ya CCM.
Maelezo ya Kinana
Kinana aliliambia gazeti hili kuwa, kulingana na
muundo wa chama hicho tawala, viongozi wanaoweza kuwahoji watu ni yeye
Katibu Mkuu, Makamu Mwenyekiti, Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri
Mkuu na Mwenyekiti wa chama Taifa. “Tena tunafanya hivyo kwenye vikao
maalumu na kwa sababu ambazo haziwezi kuwa siri.”
Kinana alieleza kuwa taarifa kwamba CCM imewahoji
watu 90 kutokana na kuwa na misimamo tofauti na chama hicho kuhusu
Serikali mbili na kura ya wazi, siyo za kweli na anaamini imesambazwa na
watu kwa malengo yao binafsi. Kinana anafafanua kuwa CCM kama chama
kikubwa nchini chenye wafuasi karibu nchi nzima, hakiwezi kudhibiti
mitizamo ya watu na kimsingi tofauti za mitazamo ndiyo msingi wa
demokrasia.
Novemba 20 mwaka 2012 akizungumza katika kipindi
cha Jenerali on Monday kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha
Channel Ten, Kinana alitoa onyo kwa makada wasaliti kuwa atasimamia
utekelezaji wa uamuzi wa Halmashuari Kuu ya CCM (Nec) ya kuwabaini na
kuwaondoa viongozi wanaokwenda kinyume na matakwa ya chama na kukipaka
matope.
Kura ya wazi na Serikali mbili
Katika hatua nyingine, Kinana alizungumzia msimamo
wa chama hicho wa kura ya siri na muundo wa Serikali mbili, akieleza
kuwa siyo jambo la ajabu, kwani katika mchakato wa kutunga katiba, kila
kundi lina maoni na mtazamo wake na kuutetea kwenye mijadala.
“Wanaosema kuna vyama havina msimamo pale bungeni
ni waongo. Siyo vyama tu, kila kikundi kina msimamo unaotokana na
uchambuzi wao wa hali ya siasa nchini na wanachofikiri kina masilahi kwa
nchi na watu wanaofuata mtazamo wao. Hawawezi kuniambia kama Lipumba
(Profesa Ibrahim) na Mbowe (Freeman), hawana wanachosimamia kwenye
mjadala huo wa Bunge Maalumu,” alisema na kusisitiza:
Alipoulizwa kama ni kweli CCM imekuwa ikiwashinikiza wajumbe wake kusimamia matakwa ya chama hicho, alijibu “Siyo CCM tu, CUF wanakutana na Chadema wanakutana, tena kila siku. Hili ni jambo la kawaida.”
Anasema tatizo siyo chama kuwa na msimamo, bali chama kutokukubali kubadili misimamo yake hata kama haikuwa sawa. Unaweza kuwa na msimamo wako, lakini ukaja mbele ya wenzako, ukagundua kuwa hauko sahihi, ikifikia hapo unapaswa kulegeza kamba ili uingize mawazo ya wenzako pia kwenye hoja zako, alisema.
Wito kwa Wajumbe wa Bunge la Katiba
“Watanzania wasitarajie miujiza, lazima mivutano ya aina hiyo
iwepo, kwani kila kundi linajitahidi kupenyeza mawazo yake na
wanaoitetea misimamo hiyo ni watu. Kikubwa hapa sasa ni uvumilivu, watu
wavumiliane na wazungumze kwa hoja na mwisho wa yote wafikie mwafaka.”
Alipoulizwa kama ni kweli CCM imekuwa ikiwashinikiza wajumbe wake kusimamia matakwa ya chama hicho, alijibu “Siyo CCM tu, CUF wanakutana na Chadema wanakutana, tena kila siku. Hili ni jambo la kawaida.”
Anasema tatizo siyo chama kuwa na msimamo, bali chama kutokukubali kubadili misimamo yake hata kama haikuwa sawa. Unaweza kuwa na msimamo wako, lakini ukaja mbele ya wenzako, ukagundua kuwa hauko sahihi, ikifikia hapo unapaswa kulegeza kamba ili uingize mawazo ya wenzako pia kwenye hoja zako, alisema.
Wito kwa Wajumbe wa Bunge la Katiba
Kinana ametoa wito kwa Wajumbe wa Bunge Maalumu la
Katiba akiwataka watambue kuwa Tanzania siyo nchi ya kwanza kutengeneza
katiba.
Alisema zipo nchi nyingi duniani, ikiwamo India,
Indonesia, Columbia, Kenya na Pakistan ambazo zilitumia muda mrefu zaidi
kutunga katiba zao.
“Sisi kutumia majuma matatu kutengeneza kanuni za
kuongoza Bunge Maalumu la Katiba, ni hatua nzuri tunayopaswa kujivunia,”
alisema.
Kinana aliendelea kueleza kuwa pamoja na tofauti
zinazojitokeza katika mijadala ya Bunge hilo Maalumu, makundi yanayounda
Bunge hilo yanapaswa kutambua utaifa na uzalendo na ikilazimika waache
tofauti zao ili wawe na mwelekeo wa pamoja katika kufikia mwafaka
unaokusudiwa.
“Kwa hali hiyo pamoja na tofauti zetu, tusiondoke
kwenye lengo. Mimi naamini katiba tunayoitaka itapatikana ila safari ya
kuipata ni ndefu na ngumu.”
0 comments:
Post a Comment