Saturday, 8 February 2014

WAFANYABIASHARA WAJIPANGA KUFANYA MGOMO KESHO

Filled under:



WAKATI uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini (JWT) wakisubiri kukutana na Rais Jakaya Kikwete, baadhi ya wafanyabiashara wameanza kusambaza ujumbe wenye kushinikiza mgomo kuanzia kesho.

Akizungumza na  Katibu wa JWT, Swed Chemchem, alikiri kuwapo kwa ujumbe huo unaowasisitiza kuacha kutumia mashine za kielektroniki za EFD zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Uongozi ulimwandikia barua rais lakini hali si ya kawaida, baadhi yetu wameanza kutuma ujumbe wenye lengo la kushinikiza mgomo,” alisema mfanyabiashara huyo.

Aliongeza kuwa ujumbe huo unaweza kuleta athari kwa Watanzania endapo wafanyabiashara wataamua kufanya mgomo huo.

Ujumbe uliosambazwa kwa wafanyabiashara hao unasema: “Wafanyabiashara wa Kariakoo na Tanzania tumeamua kutonunua mashine za EFD’s kutokana na usumbufu wake.

“…Na kwa vile serikali imekataa kuweka mfumo mzuri wa ulipaji kodi, tarehe 10 tumeazimia kufunga biashara zetu ili serikali isikie kilio cha watu wake, mashine hizi zina ufisadi mkubwa kuliko wa Richmond.”

0 comments:

Post a Comment