Wakati
Rais Jakaya Kikwete akijiandaa kwenda London Uingereza kuhudhuria
mkutano wa kuokoa viumbe vilivyo hatarini kutoweka duniani ukianza wiki
hii, tatizo la ujangili limeweka wingu zito kwa Tanzania. Rais
Kikwete ni kati ya viongozi wa nchi 50 watakaohudhuria mkutano huo,
utakaokuwa chini ya wenyeji wa mwana wa Wales na Waziri wa Mkuu wa
Uinegerza, David Cameron.
Taarifa ya gazeti la The Mail on Sunday la
Uingereza la Februari 8, limeitaja Tanzania kama kinara wa ujangili kwa
kuua zaidi ya tembo 11,000 kwa mwaka, huku Rais wake (Jakaya Kikwete)
akielezwa kufumbia macho. Pia,
gazeti hilo limemhusisha Rais Kikwete kuwa na urafiki na
wafanyabiashara ya meno ya tembo, huku likiwahusisha wafadhili wa Chama
cha Mapinduzi (CCM) katika biashara hiyo.
“Utawala
wa Rais Kikwete umetawaliwa na mauaji ya tembo yaliyovunja rekodi
katika historia ya nchi yake. Kibaya zaidi, wahifadhi wanasisitiza kuwa,
ndani ya Serikali kuna viongozi wanaoshiriki biashara hiyo,” imesema
sehemu ya taarifa hiyo. Katika
mkutano huo, viongozi wa nchi 50 na mawaziri wataweka mikakati dhidi ya
biashara haramu ya wanyamapori, yenye thamani ya pauni 6 bilioni za
Uingereza kwa mwaka zinazotumika kufadhili magaidi.
Taarifa hiyo inasema kuna wafanyabiashara wakubwa wa Dar es Salaam wanaohusika na ujangili. “Miongoni
mwao ni matajiri wakubwa nchini, wafadhili na wanachama wa CCM na
ndugu wa karibu wa Rais Kikwete. Lakini wanao marafiki wakubwa, huku
majaji, waendesha mashtaka na polisi hurubuniwa kwa urahisi,” inasema
sehemu ya taarifa hiyo.
0 comments:
Post a Comment