Monday, 10 February 2014

MADABIDA KIZIMBANI KWA KESI YA KUSAMBAZA DAWA ZA ARV FEKI NA UHUJUMU UCHUMI

Filled under:



Ofisa Mtendaji  mkuu wa Tanzania  phamarcetical industies (TPI) LTD Rhamadhani Madabida amefikishwa mahakamni kutokana na kusambaza dawa feki za Kupunguza Makali ya Virusi vya Ukimwi(ARV)

Madabida na wenzake watano,wakiwemo watumishi wa bohari kuu ya madawa(MSD) walipandishwa kizimbani mahakamaya hakimu mkazi,kisutu.

Mmiliki huyo wa TPI,ambaye ni mwenyekiti wa mkoa wa Dar es salaam na wenzake wanadaiwa kusambaza dawa hizo bandia nakuisababishia MSD hasara ya sh.148 ML

Mashitaka mengine ya kesi hiyo ni uhujumu uchumi,namba 5 ya mwaka huu,wafanyakazi  wa PTIwalioshiriki Mkurugenzi Mtendaji wa Uendeshaji,Seif Shamte,Meneja Masoko Simon Msofe,na Mhasibu Msaidizi Fatuma Shango
 
 Wafanyakazi wa MSDwalioshiriki ni meneja udhibiti ubora,Sadiki Materu,na Ofisa Uthibiti Ubora, evanse mwemezi.

0 comments:

Post a Comment