Zaidi ya watu 50 wamefariki nchini Burundi baada ya kusombwa na maji pamoja na maporomoko ya udongo.
Kwa mujibu wa waziri wa usalama, mvua kubwa ilinyesha usiku kucha katika mji mkuu Bujumbura na kusababisha uharibifu mkubwa.
Nyumba zimebomoka kufuatia mvua hiyo kubwa
Waziri Gabriel Nizigama amesema kuwa tayari
wamepata miili ya watu 50, waliofariki baada ya nyumba zao kuporomoka na
kusombwa na maji.
Mitaa na vitongoji vya mji mkuu Bujumbura viliopo kaskazini vimeathirika zaidi.
Serikali ya Burundi mbali na kutangaza kwamba
itagharamia mazishi na huduma kwa majeruhi, imetangaza pia siku moja ya
maombolezi ya kitaifa hapo kesho.
0 comments:
Post a Comment