Kutawaliwa na vinyweleo vingi mikononi na miguuni ni hali ambayo huwakera watu wengi hasa wanawake, ambao huona kuwa ni kikwazo kwao kuonekana warembo.
Wapo waliojaribu kukabiliana na kero hiyo, kwa
kutumia njia mbalimbali, hata wengine kuumia na kuiacha ngozi ya maeneo
husika ikiwa na michubuko au kuharibika na kuwasababishia madhara.
Wengi hupendelea kuviondoa vinyweleo hivyo kwa
kuvinyoa, lakini ili kupata matokeo bora, mambo mbalimbali yanatakiwa
kufuatwa ili kufanikisha zoezi hilo na kuiacha ngozi yako katika hali
nzuri.
Jambo la kwanza; hakikisha unatumia mashine yenye
wembe mpya ili kurahisisha unyoaji, kwani wembe butu utakufanya utumie
nguvu nyingi kujinyoa, hatimaye kuumiza na kujeruhi ngozi.
Kabla hujaanza kuondoa vinyweleo, hakikisha
unalowanisha eneo husika, miguu au mikono kwa muda usiopungua dakika
mbili ukitumia maji ya baridi.
Unaweza kupaka krimu ya kunyolea au kulainisha
ngozi, kisha anza kunyoa kwa kuipandisha mashine toka chini kwenda juu,
ili kufanya vinyweleo vyote vitoke kwa urahisi na kuacha ngozi ikiwa
laini bila makovu.
Tumia mkono kupapasa ili kukagua kwa umakini eneo
ulilonyoa kujua kama umeondoa vinyweleo vyote. Ikiwa bado vipo, rudia
hadi uhakikishe umevimaliza vyote.
Baada ya kumaliza, paka mafuta hususan ya maji ili
kulainisha kabisa ngozi na kuondokana na mikwaruzo. Hiyo itatoa nafasi
kwa matundu ya kupitisha hewa kwenye ngozi yako kufanya kazi yake
vizuri.
0 comments:
Post a Comment