Sunday, 16 February 2014

JE UNA TATIZO LA KUWA NA MIDOMO MIKAVU,FAHABU TIBA MBALIMBALI LA TATIZO HILO

Filled under:



UKAVU katika midomo ni tatizo, ambalo huwakabili watu wengi bila kujali jinsia wala umri.

Pamoja na kuonekana ni la kawaida, lakini hukosesha raha na kumfanya mtu ajihisi kupoteza mvuto wake.

Watu wa jinsia zote hasa wafuatiliaji wa masuala ya urembo na utanashati, huangaika mara kwa mara kutafuta njia au dawa inayoweza kuwasaidia kuondokana na tatizo hili, bila kujua nini chanzo.

Tatizo hili husababishwa na mambo kadha wa kadha, kubwa zaidi likiwa ni hali ya hewa, upepo mkali huchangia kwa kiasi kikubwa kukauka kwa midomo, hatimaye kupasuka kabisa kama hakutafanyika lolote kukabiliana na kero hiyo.

Sababu nyingine zinazoweza kuchangia kutokea kwa tatizo hili ni matumizi ya dawa, maambukizi katika midomo, matumizi ya vipodozi vyenye kemikali, kukosekana kwa virutubisho mwilini pamoja na magonjwa ya ngozi.
Namna ya kufanya
Zipo njia mbalimbali za asili, rahisi na ambazo zinaweza kukabilana na tatizo hili kwa kukinga, kupunguza na hata kumaliza kabisa ukavu  wa midomo, endapo zitafuatwa na kutumika kwa usahihi.
Zifuatazo ni miongoni mwa njia  hizo.

Unywaji wa maji
Pamoja na kukabiliana na tatizo hili maji yana umuhimu mkubwa katika mwili wa binadamu.


Katika hali ya kawaida, upungufu wa maji unaweza kuchangia kwa namna moja au nyingine kutokea kwa tatizo hilo.

Ni vyema binadamu kunywa maji yasiyopungua lita tano kwa siku, hiyo itachangia kulainisha siyo midomo tu, bali ngozi ya mwili mzima kwa ujumla.
Matunda na mboga za majani
Matunda pia hususani yenye maji maji kama karoti, matango, nyanya na matikiti yanaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kukinga au kukabiliana na tatizo hili.
Unaweza kula matunda hayo yakiwa hivyo au kwa kutengeneza juisi. Mboga za majani pia kama mchicha na spinachi unaweza kuchemsha na kunywa maji yake.
Matumizi ya lipbam
Umakini unahitajika katika uchaguzi wa mafuta ya kutumia mdomoni. Ni vyema zaidi yakatumika mafuta yenye ladha ya matunda ya kawaida na kuachana na zile zenye kemikali.

0 comments:

Post a Comment