Bunge nchini Kenya limeidhinisha mfumo mpya wa kisasa
wa kuwatambua wabunge wanaohudhuria vikao bungeni kwa kutumia alama za
vidole vyao.
Spika wa bunge amekanusha madai kuwa mojawepo wa
sababu ya kuwekwa mitambo hiyo ilikuwa ni kukabiliana na ulaghai
miongoni mwa wabunge, '' nigependa kurekebisha dhana iliyojengwa na
vyombo vya habari kwamba mitambo hii imewekwa ili kuzuia ulaghai
Mitambo hii itasaidia katika kuokoa
muda unaotumiwa na wabunge kupiga foleni ili waweze kuweka saini ya
kuingia bunge kwa njia ya kawaida.''
Kumekuwa na tuhuma kwamba wabunge wamekuwa
wakitumia afisa wa serikali kuwatilia saini kwa niaba yao ili wapate
malipo ya dola 58 ya kuhudhuria vikao hivyo.
Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa wabunge wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi duniani.
Mwandishi Sirari aliyehudhuria
uzinduzi huo katika majengo ya bunge Nairobi, ameona wabunge
wakijisajili kwa kutumia mbinu hiyo mpya kabla ya kuanza vikao vya
Jumanne ambapo wamerejea kazini tangu likizo ya Krismasi.
Wabunge hao wana hadi wiki moja kujisajili na watalazimika kutumia mashine hizo wakati wakipanga foleni kuingia bungeni.
0 comments:
Post a Comment