Mahakama nchini Kenya imemtoza faini ya shilingi milioni 20 au dola laki mbili na thelathini raia mmoja mchina kwa kuhusika na biashara haramu ya pembe za ndovu.
Adhabu hii inatokana na sheria kali za kudhibiti uwindaji wa wanyama pori.Tang Yong Jian alikamatwa wiki jana
akiwa na Pembe za Ndovu zenye kilo 3.4 katika sanduku lake katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Ikiwa atashindwa kulipa faini hiyo huenda akafungwa miaka saba gerezani.Kenya iliharamisha biashara ya pembe za Ndovu
mwaka 1989, lakini kumekuwa na ongezeko la biashara hiyo haramu katika
miaka ya hivi karibuni.
Kuna hitaji kubwa la pembe hizo barani Asia kwa
matumizi ya mapambo huku wahifadhi wa mazingira wakishuku kuwa pembe za
Vifaru hutumiwa kama dawa Mashariki mwa Bara Asia.
Nchini Kenya kilo moja ya Pembe za Ndovu, inaweza kukugharimu kati ya shilingi 12,000-18,000.
Uwindaji haramu umetajwa kama bishara haramu ya
kimataifa ambapo wawindaji hasa huwawinda ndovu na vifaru kwa wingi. Ni
hapo jana tu ambapo kifaru mmoja aliyetambulika kwa jina Josephina,
aliuawa katika mbuga ya wanyama ya Nairobi.
Kwa muda wa wiki moja nchini Kenya, kimeripotiwa matukio manne ya uwindaji haramu katika mbuga tofauti tofauti. Mkuu wa shirika la kulinda wanyama pori nchini
Kenya, bwana William Kipsang, anasema kuwa tatizo la uwindaji
linachangiwa na maswala ambayo hawawezi kudhibiti kama shirika.
''Serikali ya Kenya imetumia mamilioni ya fedha
kuhifadhi wanyama pori , lakini nchini Kenya na kwingineko barani Afrika
raia wengi wangependa kuona usalama wa binadamu ukishughulikiwa kwanza
badala ya wanyama pori.
Vile vile watu wengi huishi katika miji iliyo
mbali na misitu na wanyama hao,'' alisema Kipsang
Mashirika ya kulinda wanyama wanasema ikiwa
tatizo la uwindaji haramu halitatatuliwa, basi kwa muda wa miaka
ishirini, ndovu na vifaru barani Afrika hawatokuwepo tena.
Asilimia kumi ya uchumi wa Kenya hutegemea
utalii, ikiwa Kenya itapoteza Ndovu na vifaru wake, basi sekta ya utalii
itaathirika pakubwa
0 comments:
Post a Comment