Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wamewamamishwa kazi kwa
miezi mitatu watendaji sita wa halmashauri hiyo kwa tuhuma za ubadhilifu
wa Sh. milioni 28.
Akisoma maamuzi yaliyofikiwa na madiwani baada ya kujigeuza kuwa
kamati, Meya wa Jiji hilo, Stanslaus Mabula (Mkolani-CCM), alisema
uchunguzi wa awali umebaini kwamba watumishi sita wa halmashauri hiyo
wamebainika kutumia vitabu 'feki' na kujipatia Sh. milioni 28
ikiwa ni ushuru wa kuegesha kupitia kiwanda cha samaki cha TFP
jijini hapa.
Aliwataja watendaji hao kuwa ni mhasibu, Geofrey Liana na Mary
Mushi ambaye ni mhasibu mkuu upande wa mapato ya Halmashauri ya
Jiji la Mwanza.
Mabula alisema watuhumiwa hao wamesimamishwa kwa miezi mitatu ili kupisha uchunguzi.
Aliwataja wengine kuwa ni Mhasibu mkuu wa mapato, Labisante
Meena, mtunza vitabu vya stakabadhi za mapato, Mariam Mjema na Mhasibu
mkuu wa msaidizi wa mapato, Edwine Magera ambao Mkurugenzi ameagizwa
afikishe tuhuma zao polisi kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Kwa mujibu wa Meya, madiwani wamebaini kuwa 'uchakachuaji' huo
ulifanyika kwa nyakati tofauti kati ya Julai na Novemba mwaka jana.
Alisema kitendo hicho kilifanywa kwa kutumia stakabadhi za kitabu
kilichotolewa Agosti 10, 2007 na kurejeshwa ofisini Februari 2,
mwaka 2010.
" Katika uchunguzi wetu, madiwani tumebaini kwamba fedha hizo
zilikusanywa lakini hazikuwasilishwa katika akaunti ya Halmashauri ya
Jiji la Mwanza," alisema Mabula.
Alisema Mweka hazina amepewa onyo kali kwa vile hana muda mrefu tangu alipohamishiwa jijini hapa.
Alisema kitendo kilichofanywa na watumishi hao kimesababisha hasara na usumbufu mkubwa kwa halmashauri.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Hilda Halifa,
aliwapongeza madiwani kwa kuchukua hatua dhidi ya watendaji wasiokuwa
waadilifu kazini.
Aliahidi kuwa ofisi yake itaendelea kutoa ushirikiano kwa madiwani pamoja na vyombo
0 comments:
Post a Comment