Sitofahamu imeendelea kutanda ndani ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), baada ya juzi kulazimika kuongeza muda wa kikao cha
Kamati Kuu kusubiri uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu aliyekuwa Naibu
Katibu Mkuu wake Zitto Kabwe.
Kikao hicho kiliendelea jana kikimhoji aliyekuwa
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Dk Kitila Mkumbo, huku taarifa
nyingine zikieleza kuwa Zitto Kabwe ameendelea na msimamo wake
akituhumu chama hicho kuongozwa kwa ubabe.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho kinachofanyika
Hoteli ya Mbezi Garden jijini Dar es Salaam zinaeleza kuwa mkutano huo
ulianza saa 4:00 asubuhi kwa kujadili ajenda zilizoshindwa kujadiliwa
juzi, ambapo Dk Kitila alianza kuhojiwa saa 7:00 mchana.
Hata hivyo, taarifa hizo zinaeleza kuwa baada ya
Dk Kitila kuingia kuhojiwa, aliwaomba wajumbe amwite mwanasheria wake,
ambaye anazifahamu vyema taratibu na sheria za chama ili amsaidie kujibu
hoja.
Kazi hiyo ya Dk Kitila kutafuta mwanasheria ilichukua muda mrefu na akapatikana saa 11;00 jioni ndipo kikao kilipoanza.
Hata hivyo, kabla ya kuingia katika ukumbi huo wa
mkutano, Dk Kitila aliliambia gazeti hili kuwa atatoa ufafanuzi wa
msimamo wake baada ya kutoka ndani ya kikao hicho.
Hata hivyo, hadi saa 1:00 jioni jana alikuwa bado
ndani ya chumba cha mkutano akihojiwa, huku taarifa zaidi zikieleza kuwa
wajumbe wengi walikuwa wakimsihi Dk Kitila aombe radhi ili asamehewe,
yaishe.
Baada ya kumaliza kuhojiwa saa 1:40 usiku, Dk
Kitila alisema amemaliza kazi yake na anauachia uongozi
kutoa uamuzi wake.
Mnyika alisema kuwa kama mmoja wa watu hao
hatafika kuhojiwa mbele ya Kamati Kuu, basi chama kitachukua uamuzi
kitakachoona unafaa dhidi yake.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema, Shaaban Mwamba, juzi usiku alipata kipigo kutoka kwa maofisa
wa kikundi cha ulinzi cha chama hicho waliokuwa katika eneo ambalo
mkutano wa Kamati Kuu ulifanyika, baada ya kutuhumiwa alikuwa
akiwasiliana na wafuasi wa Zitto.
Taarifa kutoka kwa mjumbe mmoja ambaye hakupenda
jina lake litajw, ilisema kuwa mtu huyo alikuwa akichunguzwa
na maofisa wa ulinzi wa chama hicho muda mrefu, kutokana na nyendo
alizokuwa akizionyesha zilizotia shaka.
Ndipo kiongozi huyo akibebwa juu juu na maofisa hao,
huku akiulizwa aliyekuwa akiwasiliana naye ni nani, kabla ya vijana
wengine wa chama kumkamata na kumweka chini ya ulinzi, wakimtaka atoe
ufafanuzi wa alichokuwa anakifanya.
Baada ya mahojiano ya muda mfupi, kiongozi huyo
alionekana akiinuka na kwenda kunawa kwenye bomba la maji, huku
akitokwa damu mdomoni.
Taarifa zilizopatikana baadaye zilidai kuwa
kiongozi huyo alikuwa akiwasiliana na mama yake Zitto na Katibu wa
Zitto, Dk Alex na kwamba pia simu yake ilikutwa na ujumbe mfupi aliokuwa
amewaandikia watu hao.
Zoezi la kujaribu kumtafuta kiongozi huyo ili
kueleza sababu ya kupigwa kwake, lakini hakupatikana eneo la mkutano
kwa madai kuwa alikwenda hospitali kupata huduma ya kwanza, lakini
hakurudi.
Wakati suala la Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto
Kabwe na uongozi wa chama chake likiendelea kuwasumbua vichwa wapenzi wa
chama hicho, inadaiwa kuwa baadhi wa wabunge, viongozi na wazee wa
Chadema, wanataka suala hilo liishe mapema.
vyanzo vinasema kuwa baadhi ya viongozi hao walitaka Zitto aende Halmashauri
Kuu ya Chadema na kuomba msamaha ili mambo yaishe.
“Walimfuata Kitila (Dk Kitila Mkumbo) wakamwambia
amshawishi Zitto ili mambo yaishe nje ya mahakama, wanataka aende kwenye
Halmashauri Kuu kuomba radhi. Kitila akawaambia kuomba radhi kwa kosa
gani?” kiilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, Zitto alilisema kuwa
kumekuwa na jitihada mbalimbali za wazee kutaka kukiepusha chama hicho
na migogoro na kuwa amekuwa tayari kwa suala hilo. “Wazee walikuwa na
wajibu wa kuhakikisha hatufiki hapa tulipofika. Sijui kama fursa hiyo
bado ipo,” alisema Zitto.
Kuhusu uamuzi wake wa kwenda mahakamani alisema:
“Nimekwenda mahakamani kutaka haki itendeke. Chama cha kidemokrasia
kinanyima vipi mwanachama fursa ya kukata rufaa?
“Nisingekwenda mahakamani kama ningeona haki ikitendeka. Tatizo kubwa la chama chetu sasa kinaongozwa na mawazo ya kihuni na yeyote mwenye mawazo ya kujenga anaonekana msaliti.”
“Nisingekwenda mahakamani kama ningeona haki ikitendeka. Tatizo kubwa la chama chetu sasa kinaongozwa na mawazo ya kihuni na yeyote mwenye mawazo ya kujenga anaonekana msaliti.”
0 comments:
Post a Comment