CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo Kata ya Sungaji wilayani Mvomero,
kinakusudia kuwajengea uwezo Makatibu na Wenyeviti wa Vijiji na
Vitongoji wa Kata hiyo, ili wajue kuweka Kumbukumbu za Chama katika hali
nzuri.
Chama
ngazi ya kata hiyo kimesema, kinakusudia kumuomba aliyekuwa Katibu wa
Wilaya ya Mvomero, Dismas Ngeresha, ili awaelekeza Viongozi hao wa
Vijiji namna nzuri ya kuandika taarifa na kuihoji Serikali ya Kata
kiutendaji.
Akizungumza
na mwandishi Mwenyekiti wa Kata ya Sungaji, Musa Kombo, alisema, Kata
hiyo Mwaka huu imekuja kivingine ili kuhakikisha kinatunza vizuri
Kumbukumbu za Chama, zikiwemo kero zinazotolewa na wananchi.
“Kwa
kuanzia, tutamuomba aliyekuwa Katibu Mkuu Chadema Wilaya ya Mvomero,
Ngeresha, ili awanoe na kuwapa Msasa Makatibu na Wenyeviti wetu wa
Vijiji, Vitongoji wakiwemo Mabalozi, ili wajue kuandika taarifa zao.
“Tunataka
pia, Viongozi hao wapewe ueledi jinsi ya kuihoji Serikali ya Kata,
Kuandika na Kutunza taarifa muhimu za Miradi, Kero za Wananchi na Mapato
na Matumizi yanayosomwa kila baada ya miezi mitatu”. alisema Kombo.
Alisema,
Kata yake imeandaa Kikao na Viongozi wote wa Kata, Vijiji na Vitongoji
wa Chama hicho, ili kufikia muafaka wa kuendesha Semina hiyo ya
kuwajengea uwezo, ili kuhakikisha Chama katika Kata hiyo kinakwenda na
wakati.
Aidha
baadhi ya Makatibu na Wenyeviti waliohojiwa, wamempongeza Mwenekiti wa
Chama wa Kata hiyo Kombo na Kamati yake ya Utendaji, kwa kufikiri jambo
ambalo, litakitoa Chama ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Kata, hatua moja
zaidi.
0 comments:
Post a Comment