REF.CDM./HO/ZNZ/VOL .2.07/2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: MWENENDO WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KIEMBESAMAKI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA
CHADEMA imesikitishwa na mazingira yaliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni zake hizo kwa vitendo vilivyofanywa na
vijana wa chama cha mapinduzi kwa kutaka kuzuia kutumia kwa kiwanja cha mpira ambacho kilipangwa na ratiba ya Tume ya uchaguzi na kusababishia usumbufu na kuchelewesha kuanza kwa mkutano huo hadi viongozi kuingilia kati ndio vijana hao walipo ondoka na mandalizi ya mkutano huo kuendelea .
CHADEMA imesikitishwa na vurugu zilizo endeshwa na vijana hao wa CCM kwa kuivamia ofisi ya Chadema majira ya saa tano na robo za usiku jimbo la Kiembesamaki iliopo Chukwani na kung’oa mlingoti wa bendera na kuondoka na bendera yetu ya chama.
Kwa vitendo hivyo vilivyofanywa na vijana hao wa CCM imeonekana kabisa kwamab chama cha mapinduzi wameshindwa kuendesha kampeni za kistaarabu na za kiungwana ,jambo ambalo linatishia kuwepo kwa amani na utulivu katika uchaguzi huo mdogo jimbo la kiembesamaki.
CHADEMA kwa vile ni chama kinachoelewa sheria na kuheshimu sheria za nchi tayari viongozi wetu wa wilaya ya magharibi walisha liarifu jeshi la polisi katika kituo cha Mazizini wakitaka uchunguzi wa kina ufanyike na hatua za kisheria zichukuliwe ili waliohusika wafikishwe katika vyombo vya sheria .
Kwa matukio hay tunalitaka jeshi la polisi kutokufanya kazi zao kwa utashi wa kisiasa ,kwani kufanya hivyo kutalishushia hadhi jeshi hilo lakini watakua na wao tutawatuhumu kuwa wanakisaidia chama cha CCM katika kuleta vurugu katika uchaguzi mdogo wa jimbo la kiembesamaki, na kujakupeleka uvunjifu wa amani kam vile ilvyojitokeza katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu uliofanyika tarehe 16/09/2012
CHADEMA kinaamini katika chaguzi zote ni vyema vyombo vya ulinzi vikawa makini katika kutenda wajibu wao,vilevile vyama pamoja na wafuasi wao havina budi kuheshimu sheria na kanuni zote za nchi na zile za uchaguzi.
CHADEMA kinakionya chama cha CCM kiache mara moja tabia zake za kijinga na kijasusi katika kipindi hiki cha uchaguzi mdogo na kiweze kushiriki uchaguzi huo wakiwa na hoja na sio vitisho na ujangiri jambo ambalo linaweza kuhatarisha amani na utulivu tulionao vilevile kuwakosesha wananchi wa jimbo la kiembesamaki kuchagua muwakilishi wanaemtaka kwa njia ya demokrasia. CHADEMA tunaiomba ZEC nao waweze kutoa muongozo juu ya matokeo kama haya yanayo endelea.
Pamoja na hayoyaliojitokeza tunawataka viongozi wetu waendelee na kampeni kama walivyojipangia na kuwatuliza wanachama wetu wasishiriki katika vitendo vya vurugu na tuendelee na kumpigia kampeni mgombea wetu HASHIM JUMA ISSA aweze kuwa mshindi na kuwa muwakilishi wa jimbo la kiembesamaki tarehe 02/02/2014.
Wako
………………………………
DADI KOMBO MAALIM
AFISA HABARI NA UENEZI
OFISI YA MAKAO MAKUU CHADEMA
ZANZIBAR
0 comments:
Post a Comment