Sunday, 1 December 2013

VIONGOZI WA AFRIKA MASHARIKI WAANZISHA UMOJA WA FEDHA

Filled under:





Viongozi wa Jumia ya Afrika Mashariki EAC, wametia saini makubaliano ya kuanzisha mfumo wa pamoja wa fedha utakaopelekea nchi tano wanachama kuwa na sarafu moja.
Marais Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya Jakaya Kikwete wa Tanzania, Paul Kagame wa Rwanda na Pierre Nkurunziza wa Burundi walifikia makubaliano hayo wakati wa mkutano wao siku ya Jumamosi mjini Kampala. 

Kabla ya kutia saini mkataba huo Rais Kenyatta amesema "huu ni wakati wa kihistoria na muhimu kwa jumiya yetu". Mkataba huo unaanzisha awamu ya mwisho ya mataifa hayo matano kuanza kuondowa sarafu zao na kuanzisha sarafu moja ya Afrika Mashariki.

Wakati wa mkutano huo viongozi hao walitia pia sahihi mkataba wa kuanzisha Baraza la Amani na Usalama la EAC, litakaloshughulikia vitisho vya usalama katika kanda hiyo. Tayari EAC inajivunia Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja kwa wakazi milioni 135. 

 Na wakati wa mkutano huo wa 15 wa viongozi Uganda iliikabidhi Kenya uwenyekiti  jumuiya hiyo unaozunguka kwa zamu.

0 comments:

Post a Comment