NAIBU Spika wa Bunge Job Ndugai amewaomba radhi wabunge kwa madai
kuwa pipi walizopewa katika ukumbi wa Bunge zilikuwa siyo safi.
Kauli hiyo aliitoa jana wakati akitoa matangazo ndani ya ukumbi huo
muda mfupi baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
Ndugai alisema kuwa katika kikao cha juzi wabunge hao waliwekewa pipi
ambazo hazikuwa na karatasi nzuri za kufutia hatua iliyotoa taswira
mbaya.
“Ndugu zangu waheshimiwa wabunge naomba niombe radhi kama
mnavyoona
leo pipi ambapo zimeletwa katika meza zenu hazikuwa nzuri, karatasi zake
zinaonekana kuchoka lakini nimeishawaeleza makatibu hapa hilo tatizo
halitajirudiwa tena,” alisema Ndugai.
Ndugai alisema kuwa visahani vilivyowekewa pipi hizo viliambatanishwa
na karatasi za kufutia ambazo hazikuwa na muonekano mzuri kwa
watumiaji.
Katika hatua nyingine, Ndugai aliwataka wabunge kujikita katika
kuchangia mada ambazo ziko katika kamati zilizowasilisha taarifa zao
bungeni na wala sio vinginevyo.
Ndugai alitoa agizo hilo kutokana na kudai kuwa hakuwepo tangu kuanza
kwa majadiliano hayo na kulazimika kuomba maelekezo kutoka kwa makatibu
wa Bunge.
Alisema haelewi wabunge wanachojadili kutokana na kutokuwepo katika
mijadala mbalimbali ambayo ilianza tangu kuwasilishwa kwa taarifa za
kamati za kudumu za Bunge.
0 comments:
Post a Comment