MR. Blue, amekanusha kufanya utapeli nchini Kenya kama
ilivyoripotiwa katika vyombo vya Habari likiwemo Gazeti Moja nchini Kenya na
mitandao ya Kijamii, amesema kuwa kuna mtu anayetumia jina lake katika kutapeli
watu.
Mr – Blue amesema kuwa ameshangazwa
na kitendo cha kusemwa kuwa amefanya utapeli nchini Kenya “ sikuwa na show
Kenya wala nini, ni waongo tu, kuna jamaa aliniambia kuna mtu amemlipa hela
kwaajili ya kufanya show Kenya, ambaye anajiita Mr.Blue halafu hajatokea , mimi
nimewaambia wametapeliwa na watu wa kwenye mitandao, kama wana uhakika ni mimi
waje kunikamata nyumbani.” Hayo yalikuwa maneno ya Mr Blue alipokuwa akifanyiwa
mahojiano na Bongo5.
0 comments:
Post a Comment