Jaji wa mahakama kuu ya Afrika Kusini Thokozile
Masipa anaendelea hii leo kutoa hukumu yake dhidi ya kesi ya mauaji
inayomkabili mwanariadha wa Olimpiki Oscar Pistorius huko Afrika Kusini.
Tayari amemuondolea makosa ya mauaji, na badala yake Pistorious anakabiliwa na makosa ya kuua bila kukusudia.
Katika
uamuzi wake huo wa kumuondolea Mwanariadha Oscar Pistorius mashtaka ya
mauaji ,jaji Thokozile Masipa alisema mwendesha mashtaka hakuthibitisha
kesi yake pasi na shaka yoyote.
Hata hivyo itabainika vyema baadae
leo iwapo atapatikana na hatia ya mauji pasi na kukusudia wakati jaji
atapoitolea kesi hiyo hukumu yakini.
Pistorius amekana mashtaka ya
kumua aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp hapo mwaka jana katika siku
ya wapendao Valentine day pale alipomfyatulia risasi kumuua.
Mwendesa mashtaka amekuwa
akisisitiza kuwa Pistorius alimpiga risasi Reeva wakati wa ugomvi baina
yao lakini Pistorius amekuwa akijitetea kuwa alidhani ni mwizi
aliyevamia nyumba yake.
Jaji amesema wakati wa tukio hilo Pistorius alikosa makini kwa kutumia bunduki yake vibaya.
Mwandishi
wetu wa Afrika kusini anasema uamuzi huu wa awali umewashangaza wengi
waliokuwa wakifuatilia kesi hii kwa karibu wakisema inavyoelekea anaweza
kupewa kifungo chepesi.
Anaepatikana na hatia la Kosa la kuuwa
bila kukusudia hupewa kifungo kisichozidi miaka kumi na tano jela na pia
kuna uwezekano wa kutumikia baadhi ya mda huo kifungo cha nje.
Hata hivyo mbali na uwezekano wa rufaa baada ya hukumu anakabiliwa pia na shtaka la matumizi mabaya ya bunduki
0 comments:
Post a Comment