Kipindi cha ujauzito wanawake wengi hujikuta wakiacha kuzingatia hatua mbalimbali za kujitunza ili kubaki warembo, matokeo yake hupoteza mvuto.
Hali hiyo inaweza kuendelea hata baada ya
kujifungua na huenda ikawa mbaya zaidi kwa kuwa mara nyingi kipindi
hicho mama hujikuta akitumia muda mwingi kumwangalia mtoto.
Kujifungua au ujauzito haiwezi kuwa sababu ya
mwanamke kupoteza urembo uliokuwanao awali. Hivyo ni jukumu la mwanamke
mjamzito au aliyejifungua kuhakikisha anabaki na mvuto wake ukiwa kwenye
kiwango stahiki.
Kuwa mrembo siyo lazima upake vipodozi vyenye
kemikali kwani vinaweza kumsababishia madhara mtoto kwa kuwa atatumia
muda mrefu akiwa mwilini kwako.
Katika kipindi hiki mama mjamzito au aliyejifungua
anatakiwa kuepuka kupaka mafuta, losheni au manukato yenye harufu kali
inayoweza kuwa na madhara kwa mtoto hata kumsabishia wakati mgumu katika
kupumua.
Ni vyema utumie vipodozi visivyo na kemikali ili
kujilinda usipoteze mvuto wako. Pia tumia muda mwingi kufanya mazoezi
mepesi yatakayoweza kukusadia kutengeneza umbile (shape), yako na
kuifanya ionekane yenye mvuto wa hali ya juu hata ikiwa umetoka
kujifungua.
Hakikisha pia kucha zako zinakuwa fupi na safi,
hii haimaanishi kwamba huruhusiwi kupaka rangi unaweza kuziremba kwa
mtindo wowote unaopenda lakini ziwe katika kiwango ambacho hakitamdhuru
mtoto kwa namna yoyote.
Kitu muhimu cha kuzingatia katika kipindi hicho ni
usafi na mwonekano wa ndani na nje. Kwa kufanya hivyo, hata mtoto
atakuwa katika mazingira salama yanaweza kumtamanisha mtu mwingine
kutaka kumshika.
0 comments:
Post a Comment