Kesi imeanza nchini Sudan Kusini ya vigogo wanne wa
kisiasa wanaotuhumiwa kwa uhaini kwa madai ya kujaribu kumwondoa
mamlakani Rais Salva Kiir baada ya vita kuzuka mwaka jana.
Washitakiwa ni pamoja na Pagan Amum, aliyekuwa
katibu mkuu wa chama tawala , mawaziri wa zamani na walinzi pamoja na
balozi wa zamani nchini Marekani.
Wote wamekanusha madai hayo.
Maelfu ya watu wameuawa katika vita kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wanaomuunga mkono Riek Machar.
Makabiliano yameendelea licha ya makubaliano ya kusitisha vita kufikiwa mwezi Januari.
0 comments:
Post a Comment