Saturday, 1 March 2014

RAY C AFUNGUA TAASISI YA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA

Filled under:



MWANADADA aliyewahi kung’ara katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema moja ya sababu iliyomfanya kuanzisha taasisi yake ya ‘Ray C Foundation’ ni kutaka kuelimisha vijana na jamii nzima juu ya madhara ya utumiaji wa dawa za kulevya na athari zake.
 
Ray C kupitia mtandao wa Instagram, aliandika kuwa kutokana na vijana wengi kujiingiza katika matumizi ya dawa hizo, ameamua kufungua asasi hiyo ili kuwaelimisha na kutambua madhara ya matumizi yake.

Alisema matatizo anayoyapata mtumiaji wa dawa hizo ni makubwa, ambayo hayazungumziki, ndiyo maana ameamua kuhamasisha jamii inayomzunguka kuyaepuka.

0 comments:

Post a Comment