Miguu kama sehemu nyingine za mwili isipoangaliwa vizuri huweza leta
madhara kiafya. Ni vizuri miguu ikatunzwa vizuri kuanzia viatu
vinavyovaliwa hadi jinsi ya kuisafisha. Kuna aina mbalimbali za viatu
mfano viatu vya kufunika vifupi, viatu virefu vya wazi, viatu vifupi vya
wazi na viati virefu vya kufunika. Viatu vyote hivi huwa vinakuwa na
muundo tofauti kadiri mvaaji anavyopendelea.
Ni vizuri kuepuka kuvaa viatu virefu sana mara kwa mara na hasa kama
unatembea navyo kwa muda mrefu maana husababisha matatizo kwenye misuli
ya miguu kama vikivaliwa mara kwa mara na kwa muda mrefu. Pia ni vyema
kutovaa viatu vya kufunika na vyenye joto sana kwa muda mrefu hasa
sehemu zenye joto kali maana huweza leta matatizo kwenye miguu. Vile
vile si vyema kuvaa viatu vya wazi nje kama sehemu inabaridi kali na
barafu.
Ili miguu yako iweze kuwa na uzuri wa asili siku zote basi ni vizuri
angalau mara moja kwa wiki uwe na siku maalumu ya kusafisha miguu yako
(sio kwamba siku nyingine husafishi, la hasha hapa naongelea usafi
maalum). Andaa maji ya uvuguvugu na uweke nyenye beseni pamoja na sabuni
ya maji na chumvi,iloeke kwa muda wa dakika 10 isugue taratibu ili kuondoa mabaki ya ngozi iliyokufa. Kisha kata kucha zako vizuri na
kama utapendelea basi uisugue miguu yako kwa kutumia mafuta maalumu ya
kusugulia kuanzia kwenye magoti hadi vidoleni (scrub).Kisha loweka
kwenye maji kwa muda wa dakika tano.
Baada ya hapo nawa vizuri na kusugua unyayo kwa kifaa maalumu au jiwe
laini kisha suuza miguu yako na maji safi. Baada ya hapo kausha vizuri
na upake mafuta mazuri kwa ajili ya kulinda ngozi ya miguu. Hakikisha
uchafu wote umetoka na hasa kwenye kucha na vidole.
Tunza miguu yako vizuri maana ni zawadi kutoka kwa Mungu.
0 comments:
Post a Comment