OFISI ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imepiga marufuku uvaaji wa nguo yoyote inayopingana na maadili ya utumishi wa umma.
Kwa mujibu wa waraka huo uliosambazwa kwenye ofisi mbalimbali nchini,
utawalenga watumishi wa umma wote na wananchi wanaohitaji kupata huduma
katika ofisi hizo.
Mavazi yaliyopigwa marufuku kwa wanaume ni nguo zenye maandishi ya
chama chochote cha siasa na yenye kuonyesha ushabiki wa kitu fulani.
Nguo nyingine ni za kazi maalumu kama vile za michezo, zenye michoro,
maandishi, picha ambazo haziendani na shughuli za serikali, zinazobana,
kaptura ya aina yoyote, suruali inayoachwa bila kupindwa, suruali ya
‘Jeans’ na fulana.
Kwa upande wa wanawake, nguo zilizopigwa marufuku ni zinazobana, fupi
zinazoacha magoti wazi, zinazoacha sehemu ya mwili wazi kama vile
kitovu na kifua na kaptura aina yoyote ikiwemo pedo na pens.
Marufuku hiyo inatokana na Mwongozo wa mavazi kwa watumishi wa umma,
kwa mujibu wa Waraka wa Utumishi wa Umma Na. 3 wa mwaka 2007.
0 comments:
Post a Comment