Thursday, 9 January 2014

TIBAIJUKA AZOMEWA NA WANANCHI KAPUNGA

Filled under:



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alipata wakati mgumu juzi jioni baada ya kuzomewa na wananchi waliokerwa na kitendo chake cha kubadilika na kumruhusu mwekezaji kuendelea kumiliki eneo la ardhi katika Shamba la Kapunga, Wilaya ya Mbarali, Mbeya.
 
Ilibidi Mkuu wa Wilaya hiyo, Gulam Hussein Kifu aingilie kati kuwatuliza wananchi hao waliokuwa wakipiga kelele na kutoa maneno makali kwa waziri huyo.
Profesa Tibaijuka alikwenda huko kwa nia ya kusuluhisha mgogoro wa ardhi wa muda mrefu baina ya wananchi wa Kapunga na mwekezaji wa Kampuni ya Kapunga Rice Project. Awali, shamba hilo lilikuwa mali ya Kampuni ya Taifa ya Kilimo (Nafco).
Wananchi hao walikasirishwa na hatua yake ya kuamua kuwa eneo hilo ni halali kwa mwekezaji huyo tofauti na msimamo wake wa awali wa kutaka ardhi hiyo irudishwe kwa wananchi.
Profesa Tibaijuka alibadili mawazo yake baada ya kufanya mazungumzo na mwekezaji huyo ndani ya gari akiwa na Mkuu wa Wilaya.
Msimamo awali
Profesa Tibaijuka alifika Kijiji cha Kapunga saa 6.45 mchana na kuanza kikao cha ndani na viongozi wa kijiji kwenye ofisi yao hadi saa 8.14 mchana. Alielezwa alielezwa kwamba mgogoro huo unatokana na kitendo vya mwekezaji huyo kutaka kupora ardhi yote ya kijiji chenye wakazi wapatao 4,400.
Mwenyekiti wa Kijiji, John Nyoni alisema mwaka 1995, wanakijiji walitoa hekta 5,500 za ardhi kwa Nafco ambazo ziko kwenye mradi maalumu wa kuendelea kilimo cha mpunga, lakini wanachoshangaa ni kuona aliyerithi eneo hilo (mwekezaji) anadai hekta nyingine 1,870 kutoka kwenye mashamba ya wananchi pamoja na kijiji chote.
Nyoni alidai kuwa katika harakati hizo, mwekezaji huyo alipokonya shule, zahanati ya kijiji na sasa anataka kuwaondoa wananchi wote. Akizungumza katika kikao hicho, Profesa Tibaijuka alisema alifika hapo kutoa jawabu la suluhisho na kwamba atakachotoa ni cha mwisho wala hakutakuwa na mgogoro mwingine tena.
“Serikali imetambua chanzo cha makosa ni Nafco kusajili na kupata hati moja kwa eneo lote likiwamo la kijiji pamoja, hivyo mwekezaji huyo alikabidhiwa hati hiyo ikionyesha eneo la hekta 7,370 badala ya hekta 5,500,’’ alisema Profesa Tibaijuka.
Aliwahakikishia viongozi wa kijiji hicho chenye vitongoji saba kwamba alifika hapo ili kumtaka mwekezaji akabidhi hati hiyo serikalini ili ofisi yake ikaibadilishe na kwamba kama atakataa atamwandikia Rais Jakaya Kikwete kumtaka aifute hati yote.

Baada ya kikao hicho, Waziri akiwa na msafara wake pamoja na baadhi ya viongozi wa kijiji walikwenda kwenye eneo la mwekezaji na kumkuta Mkurugenzi Mtendaji, Justin Vermaak ambaye alisema anawashangaa wananchi wanaokaa eneo hilo ambalo ni lake kisheria.
Vermaak alisema hati aliyonayo inaonyesha kuwa eneo lote ni lake, lakini wananchi wanakataa na matokeo yake wanasababisha vurugu.
Akizungumza baada ya kupata taarifa hiyo, Profesa alimweleza mwekezaji huyo kwamba kimsingi wananchi wa Kapunga waliipatia Nafco hekta 5,500 ambazo ndizo anazotakiwa kumiliki mwekezaji. Alisema Nafco walifanya makosa katika usajili wa hati kwa kuchanganya eneo la mashamba ya wananchi na eneo la kijiji chote.
“Hivyo tunakuomba usalimishe hati hiyo ili tukaiandike upya kwa kuzingatia eneo la hekta 5,500 na eneo jingine la hekta 1,870 kuwaachia wananchi,’’ alisema.
Mwekezaji huyo alikubaliana na uamuzi huo wa Waziri lakini akazua dai jipya la fidia... “Fidia ya nini? Kwanza miundombinu yote uliikuta na nadhani watu wa kukulipa ni wale waliokuuzia,” Profesa Tibaijuka alimjibu.
Kuona hivyo, mwekezaji huyo akaibua hoja nyingine mpya ya kutaka ardhi nyingine lakini Profesa Tibaijuka alipinga hoja hiyo na kumsisitizia kuwa awasilishe hati.
Baada ya kuona Profesa Tibaijuka anazidi kuwa mkali, mwekezaji huyo akamwomba waziri: “Basi tutaongea kwenye gari. Tupande pamoja wakati wa kuzunguka kwenye mashamba yangu.”
Waziri huyo naye alikubali kupanda gari hilo na walianza safari ya kulitembelea shamba hilo huku akiwa amepanda gari la mwekezaji huyo.
Katika gari hilo, mwekezaji alikuwa akiendesha wakati waziri akiwa mbele na nyuma yake alikaa Mkuu wa Wilaya, Kiffu na msaidizi wa mwekezaji aliyetajwa kwa jina moja la Jacob.

Abadili msimamo

Baada ya safari hiyo, waandishi walimwomba waziri atoe kauli ya Serikali kuhusu mgogoro huo ndipo aliposema kwamba baada ya kuzunguka ameona mwekezaji hana matatizo na amegundua kuwa chanzo cha mgogoro ni Serikali.
“Hivyo, Serikali itaendelea kuzungumza na mwekezaji na wananchi ili kumaliza mgogoro. Mwekezaji ni mzuri lakini wapo wananchi wakorofi ambao wanadiriki hata kwenda kuzuia maji yasije kwa mwekezaji na wanakijiji pia wana makosa,” alisema Profesa Tibaijuka.

Alipoulizwa imekuwaje amebadili msimamo wake wa awali wa kumtaka mwekezaji asalimishe hati, Profesa Tibaijuka alicheka kisha kueleza kuwa amemwelewa mwekezaji. Alipoulizwa ikiwa mwekezaji huyo atakabidhi hati kama alivyomwagiza, Tibaijuka alijibu; “Aaaah, hilo siyo la msingi. La muhimu ni kwamba mambo yanakwenda vizuri na majibu kamili yatatolewa hivi karibuni.”

Kuzomewa
Profesa Tibaijuka na msafara walianza mkutano wa hadhara na wanakijiji saa 11.45 jioni na kuwahutubia wananchi kwa kuwaeleza mwekezaji hakuwa na makosa, bali Nafco ndiyo wa kulaumiwa.
Kauli hiyo ilifuatiwa na zomea zomea huku baadhi ya wananchi wakisema: “Ondoka, umekuja kutembea huku, hujaja kutusaidia.”
Wananchi walikuwa wakisema hayo kwa sauti kubwa wengine wamshutumu mwekezaji huyo kuwa hana ushirikiano. Wamedai pia kwamba ujio wake umesababisha mateso kwa kuwa baadhi ya nyumba zao zimechomwa moto na wengine mazao yao kunyunyuziwa sumu katika kipindi hiki cha mgogoro. Wakati wengine wakilalamika na kusema kila mmoja lake, wapo waliokuwa wakinyoosha mikono wakitaka kupewa nafasi kutoa madukuduku yao mbele ya waziri huyo.
Hali hiyo kukosekana uelewano baina ya waziri na wananchi hao ilimfanya Mkuu wa Wilaya kuingilia kati na kuwaomba wananchi hao

0 comments:

Post a Comment