Kamishna wa wilaya katika eneo la Kilimanjaro (Herman Kapufi,)
amesema kuwa watu 38 waliokamatwa Jumatatu miongoni mwao ni wazazi wa
wasichana waliokuwa wanakeketwa.
Alisema kuwa wasichana waliokeketwa wanapokea matibabu.
Maafisa wakuu mjini Moshi Tanzania, waliwakamata
wanawake 38 mnamo siku ya Jumatatu waliopatikana wakiwakeketa wasichana
katika eneo hilo.
Haijulikani idadi ya wasichana walioathirika. Lakini ripoti zinasema kuwa walikuwa kati ya umri wa miaka 3 na 16.
Ingawa ukeketaji ambao umeharamishwa huendelezwa
katika sehemu nyingi za Mara na Dodoma nchini Tanzania , hilo sio jambo
la kawaida kutokea mjini Moshi.
Inaarifiwa wanawake hao walikamatwa walipokuwa
wanacheza dansi ya kitamaduni wakiwazingira wasichana ambao ndio
walikuwa wamekeketwa tu.
Baadhi ya wasichana inaarifiwa bado walikuwa wanavuja damu na wengine wakiwa wanauguza majeraha.
Ukeketaji umeharamishwa nchini Tanzania tangu mwaka 1998 ingawa bado unaendelezwa katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo.
Inakisiwa asilimia 15 ya wasichana pamoja na wanawake wamekeketwa nchini humo.
0 comments:
Post a Comment